Wazalishaji wa pedi waitupia lawama serikali

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Wazalishaji wa pedi waitupia lawama serikali https://www.jamiiforums.com/index.p...ikali&format=pdf&option=com_content&Itemid=57https://www.jamiiforums.com/index.p...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57https://www.jamiiforums.com/index.p...hbGkmb3B0aW9uPWNvbV9jb250ZW50Jkl0ZW1pZD01Nw==
Friday, 29 January 2010 06:35
Na Edmund Mihale
Majira

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Kays Hygene inayotengeneza pedi aina ya Jessy, Bi. Khadija Simba ameitupia lawama serikali kwa kushindwa kusimamia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya hapa nchini, hali inayosababisha nchi kuwa dampo la kuuzia bidhaa bandia.

Kauli hiyo imekuja siku mbili baada ya polisi kukamata pedi bandia aina ya Always zenye thamani ya sh. milioni 60 zilizokuwa zikisafirishwa kwenda mikoani.

Akizungumza na Majira ofisi kwake Dar es Salaam jana, Bi. Simba alisema Watanzania wengi wamekata tamaa katika kuanzisha viwanda, hivyo wameamua kuwa wachuuzi wa bidhaa za nje husasni katika nchi ya China kutokana na unafuu wa bei zake.

"Kuna udhaifu mkubwa kwa watendaji wa serikali na sisi wenyewe katika kusimamia wawekezaji wa ndani kwa kuwa tumekosa uzalendo wa kuipenda nchi yetu," alisema Bi. Simba.

Alisema serikali kushindwa kuteteta viwanda vya hapa nchini ni sawa na kuwamilikisha wageni uchumi na kuwacha wazawa mkono matupu, hali ambayo ni hatari kwa taifa la leo na vizazi vijavyo.

Alisema watendaji wengi wa serikali na wafanyabishara wasio na mapenzi na nchi yao, wamekuwa wakiangalia maslahi ya sasa bila kujali ya kesho na vizazi vijavyo kwa kuingiza bidhaa ambazo ni hatari kwa Watanzania kutokana na kusababisha magonjwa yasiyopona.

Wakati lawama hizo zikitolewa, taarifa za kitaalamu kuhusu bidhaa hizo bandia zinasema kuwa zinasababisha madhara makubwa kwa akina mama, yakiwamo magonjwa ya fangasi na maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI).
 
He! hatari hii sasa,

'udhungu' huu bwana

Hali ikiwa mbaya serikali inabidi iingilie kati watu warudi kwenye vipande vya kanga! LOL!

hata Jessy nazo wajanja wakitaka watazicopy tu,

mpaka pedi watu wanafoji!!!,

inabidi wanaume tusaidie kukagua pedi za wake zetu sasa kama ni genuine maana mambo yakiharibika - khatari!

nawalaani wezi hawa wanaotaka kuharibu maisha ya watu na hasa wanaume

Lol!
 
Iko kazi...sijui tuwashauri wake zetu waache kutumia pedi..warudi kwemye matambala..siunajua mambo ya asili yalivyo mazuri...
 
Iko kazi...sijui tuwashauri wake zetu waache kutumia pedi..warudi kwemye matambala..siunajua mambo ya asili yalivyo mazuri...
kweli mkuu ila ukiangalia kwa nyakati zetu hizi inamana hatatoka tena out mpaka amalize mzunguko je wataweza tupambane tu na feki
 
hii inanikumbusha mbali kuna mtu mmoja alikuwa akiiingia mwezini anabadilisha mwendo
 
vipande vya kanga vipo durable kuliko "always" ila sasa watapoteza mazavi.....
 
Back
Top Bottom