Wayne Rooney atangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa Uingereza

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Wayne Rooney ametangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Uingereza, ameichezea michezo 119 na kufunga magoli 53.

Rooney.jpg
 
nafikiri ameangalia mbali zaidi miezi ile iliyopita aliitwa halafu akawaanakalia benchi wayne amewaza huyu mwalimu hanipendi sasa ilitusigombane na kuvunja heshima yangu ni bora nitangaze mapema!!kwanza ni kiongozi amewaza makosa ya miezi iliyopita ovaaa
 
Rooney ni sehemu ya mradi kabambe na mkubwa ulobuniwa na mmoja wa wamiliki wa timu ya Everton Farhad Moshiri.

Wanaiandaa Everton ije kuwa timu kubwa pinzani kwa Liverpool na timu zingine kubwa nchini humo.

Sasa ukiwa ni mtu kama Wayne Rooney au meneja Ronald Koeman kwenye chumba cha wachezaji morali inakuwa siku zote ipo juu na kama unaifuatilia timu hiyosiku ya jumatatu ilitoka sare na Machester City katika uwanja wa Etihad na mfungaji wa goli la kuongoza kwa Everton akiwa Wayne Rooney.

Moshiri ana hisa asilimia 49.9 kwenye timu hiyo.

Walimshawishi ajiunge na Everton na badala ya kwenda Uchina abakie Uingereza kama alivyofanya John terry ambae naye amejiunga na timu ya daraja la pili Aston Villa.

Rooney na John Terry wote ni manahodha wa timu hizo za Uingereza ambazo zote zina wawekezaji wa kutoka Uchina,

Timu za Everton, Tottenham Hotspurs na Liverpool kwa sasa ni timu zinazotishia ustaarabu wa timu kama ya kwangu Arsenal, Manchester United na Chelsea.

Tuziangalie timu hizi katika ligi ya msimu huu na kuna ushindani mkubwa kuanzia ni nani wanasajiliwa mpaka katika mechi zenyewe.
 
Back
Top Bottom