Kkiukweli mimi ni shabiki wa simba lakini nilitegemea kuwa usajili wa kwanza simba kwenye dirisha dogo ni golikipa lakini si kiungo kwani wapo wa kutosha. Dhaira hatabiriki kama mvua za vuli kuna siku yupo vizuri kuna wakati anakuwa kama shati. Huyo andrew ntalla kibadeni anajua kwa nini alaimsajili simba lakini sio kipa mwenye hadhi ya kuchezea simba. Yule dogo hashim abuu ni mzuri sana ila anahitaji kama miaka miwili ya uzoefu apate mechi za mara kwa mara atatisha. Kwa sasa simba inahitaji kipa mzoefu kwa hararka na kama sio chuki binafsi kaseja alitakiwa aendelee kuwepo simba then huyo dogo angemrithi vizuri.
Zungumzia Ya Timu Yako ya KUBEBWA KIMBELEKO ( Yanga ) na Ya Simba Sports Club Tuachie Mwenyewe na Huo Usajili ni Mzuri mno kwani Simba ilihitaji Kiungo anayefanana na Mentor Wangu na Kipenzi Changu Kiungo wa Karne na Wa Rekodi Simba Suleiman Abdallah Matola ( Veron / Mzambia ) na Huyu Awadh Juma anahidhi na Atatusaidia Sana Kwani Hatuna Kiungo anayeweza Kumlisha Mipira na Kumchezesha Vizuri Amis Tambwe na Nina Uhakika Tambwe sasa Atakuwa Anacheka tu na Nyavu na Simba Pia tulikosa Wing Midfielder ambaye Anaweza Kupunguza Kijiji Kama Ilivyokuwa Kwa Emanuel Okwi na huyu Dogo Ally Badru ni Aina ya Okwi na atakuwa Anamchezesha Sana Betram Mwombeki Mbelwa. Simba hatusajili kwa Kukomoa au Sifa na Tunasajili Kwa Malengo na Mahitaji Muhimu na MTAIPENDA TU!
ukweli huu hawautaki wenzio
ni kweli amavubi mara nyingi ushabiki unatufanya tuwe vipofu na ndio maana kila siku tunadanganywa mara uwanja bunju, mara sunderland, n.k. Yanga wamesajili wachezaji 2 haraka haraka rage naye anasajili 2 kutudanganya wakati ukweli kwa mtu anayejua mpira na aliyeiona simba mwaka huu anajua timu ni nzuri ila tatizo ni golikipa na makocha kwani timu haijulikani inacheza mfumo gani. Kocha amekaa na timu zaidi miezi miwili na ligi kacheza mechi 10 na bado anakwambia hajapata first eleven mara ohh timu hii naijenga ya miaka 2 ijayo. Simba ya msimu uliopita ilikuwa nzuri tatizo lilikuwa mabeki wa kati wao wakamtimua kaseja baada ya kusajili mabeki wazuri wa kati na kuleta shati jipya golini toka uganda.
"Mwenyekiti huyo alikiri kuwa Ally Badru Ally waliyemsajili kutoka Suez Canal ya Misri hakuwapo kwenye mipango yao, lakini kwa sababu alikuwapo tu Dar es Salaam wanaamini kuwa atawasaidia katika ushambuliaji."....... nukuu toka kwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba kupitia gazeti la Mwanaspoti. Mchezaji anasajiliwa si kwa mahitaji ya timu bali kwa sababu yupo tu Dar es Salaam, ama kweli bongo bado lala!
Kwani Amis Tambwe na yule mwenzake yuleee Mwombeki vipi tena sio washambuliaji wale??
ni vyema kuwa na mbadala, uko sahihi