Wawili Watua Simba

Wawili Watua Simba

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Na Mahmoud Zubeiry, Samora
SIMBA SC imesajili wachezaji wawili kwa mpigo leo hii, kiungo mchezeshaji Awadh Juma Issa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na Ally Badru Ally kutoka Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri.
Wachezaji hao wawili wa timu ya soka ya taifa ya Zanzibar wamesaini adhuhuri ya leo, nyumbani kwa Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Rage (katikati) akiwa na Badru Ally kulia na Awadh Juma kushoto nyumbani kwake leo baada ya kuwasaini.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Walitua kwa ndege maalum na mchana wakaenda kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja na baada ya hapo, wakarejea kwenye kambi ya Zanzibar Heroes inayojiandaa na michuano ya CECAFA Challenge.
Akizungumza baada ya kuwasajili wachezaji hao, Rage ambaye ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini (CCM), alisema kwamba usajili huo umetokana na mapendekezo ya benchi la Ufundi.
“Ni wachezaji wazuri, ambao tunawajua vizuri na tumekuwa tukiwafuatilia kwa muda mrefu na tuna imani nao sana kwamba watakuja kuisaidia timu yetu,”alisema Rage.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Awadh Juma akitia dole gumba pembeni ya Alhaj Rage[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Awadh Juma akiwa ameshika kwa pamoja na Rage Mkataba wake[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Badru akisaini pembeni ya Alhaj Rage[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Badru akiwa ameshika kwa pamoja na Rage Mkataba wake[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Badru akisaini kurasa za Mkataba [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Msomi; Katibu Mkuu wa Simba SC, Evodius Mtawala akiupitia Mkataba aliouandaa kabla ya kuuchapisha ili wachezaji hao wasaini [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kwa upande wake, Badru alisema kwamba amefurahi sana kusaini Simba SC na anaamini nyota yake itang’ara huko. “Simba SC ni timu kubwa, maarufu, naamini kabisa hapa nitafanya vizuri, kikubwa tu naomba sapoti ya mashabiki wote,”alisema.
Kuhusu klabu yake ya Misri aliyoichezea tangu mwaka 2010, Badru alisema kwamba imemruhusu kuondoka ingawa alikuwa ana miaka miwili zaidi katika Mkataba wake na klabu hiyo.
Juma ambaye ameichezea Mtibwa Sugar kwa miaka miwili tangu alipojiunga nayo akitokea Taasisi ya Soka Tanzania (TSA) ambako alikuwa pamoja na Thomas Ulimwengu alisema kwamba amefurahi kutua Msimbazi.
“Nimefurahi sana kuja Simba SC, ni ndoto zangu za muda mrefu na sasa ni wakati wa kufanya kazi tu,”alisema.
 
4w09DREFXREFX9DMPlfSnI6ZsIKZsIKb8REz5iYiC7v8BhfO4t41SMGAAAAAASUVORK5CYII=
 
Hivi huyu mchezaji akija kukana Rage atasema nn? natumai mmenielewa
 
Unasema!!!??? Kuna mazingatio hapo kwenye comment yako

ni angalizo tu, halafu ukisoma wachezaji wenyewe, mmoja anasema ana mktaba wa miaka miwili huko Arabuni, mweininge ni mchezaji wa Mtibwa na hatujui kama hana mkataba au la........majanga tu
 
ni angalizo tu, halafu ukisoma wachezaji wenyewe, mmoja anasema ana mktaba wa miaka miwili huko Arabuni, mweininge ni mchezaji wa Mtibwa na hatujui kama hana mkataba au la........majanga tu

Mean za kupata stress enh!
 
Wapemba na mpira wapi na wapi bhana? Ni Chollo na Canavaro tu ndio walijaaliwa bahati hiyo.
 
Wapemba na mpira wapi na wapi bhana? Ni Chollo na Canavaro tu ndio walijaaliwa bahati hiyo.
Awadh anajuajua, nimeshamuona Mtibwa, huyu mwingine sina uhakika, lakn waswahili wanasema maji hayapandi mlima
 
Mwenyekiti wangu keshakosa sifa ya kuaminiwa, aliwahi kutuletea picha akiwa na Mrundi mmoja mwaka jana matokeo yake watani wakamchukua.
 
Mwenyekiti wangu keshakosa sifa ya kuaminiwa, aliwahi kutuletea picha akiwa na Mrundi mmoja mwaka jana matokeo yake watani wakamchukua.

Naipenda Simba lakn Rage ni mtu wa propaganda tu
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Hawa wachezaji kama walifanyiwa Scouting na kujua viwango vyao, hongera mwenyekiti ila kama wamerajiriwa kwa story kwamba ni wachezaji wazuri itakuwa hasara kwa timu
 
Hawa wachezaji kama walifanyiwa Scouting na kujua viwango vyao, hongera mwenyekiti ila kama wamerajiriwa kwa story kwamba ni wachezaji wazuri itakuwa hasara kwa timu

Ninachojiuliza, iweje wachezaji wakasajiliwe nyumbani kwa Mwenyekiti tena siku ya Jumapili, nahisi Rage anatafuta Kura hapa.........
 
Back
Top Bottom