Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Nimependa jinsi wanavyorudisha maadili huko arumeru....hakuna kuvaa nguo ukaishusha chini ya makalio---,kuvaa vimini na suruali kwa wanawake,unywaji wa pombe wakati wa kazi...na hata ukinywa unywe kistaarabu sio kusumbua wenzako kwa kelele hii ni hata kama upo kwako.aisee watu wanachezea fimbo kwa kwenda mbele unachabangwa fimbo 60-70.
 
Kwanza, niupongeze kwa dhati uongozi huo wa kijiji. Ni nadra siku hizi viongozi wakikerwa na shida ktk jamii wanachukua hatua, wengi ni kulaumu na kulalama tu!

Kisheria mamlaka waliyonayo viongozi wa vijiji inawaruhusu kutunga sheria ndogondogo kusimamia utawala wao. Hili wala siyo la kwanza, Manispaa ya Moshi ukitupa taka faini papo kwa hapo, ila Temeke popote ni dampo!! Miji yote inaiga Moshi, kwa hiyo vijiji vingine vikiiga sii baya. Kama unawaona Arusha wamekaza sana, nenda Zenji na kipedo au kata K. ..... Sitaki kuwa shahidi mie!!

Kuna mtu humu anauliza nafasi ya wakuu wa dini kuhukumu, eti wao hawana dhambi? Kwani nani alikuambia hakimu ni mtakatifu, si naye anahukumu? Tena wangine kifo na wananyongwa?

Ukienda kwa watu, uliza kwanza!!
 
Nauliza ivi waafrika kabla ya wazungu kuleta nguo za pamba na sufi walikuwa wanavaa nn, na kwa nn tusirudie asili yetu ya mavazi
 
Yan ni tabu tupu lakin ukiwauliza wanasema maadili yamepotea xo wanataka maadili ya kimeru yarudi km zamani! me nlikuwa hme likizo yan ni fulu kanga hta ukitaka kutoka hamna suruali wala nn!ntafanyaje xx na ndo kwetu inabidi utii mamlaka iliyowekwa cz hta vitabu vitakatifu vinasema hvyo!
 
This is against human rights how can you decide for others we have to let people live their lives YOLO

Uwe makini na Hiki kitu haki za binadamu. Kila mtu akipewa uhuru unaojaribu kuutetea. Labda nikuulize: kwa nini utamshtaki au kumuua atakayekuibia? Je, uko tayari kupokea mahari ya kaka yako "akiolewa"? Nao ni haki zao!!??!!
 
Kuingilia Uhuru Wa MTU sio issue...kila MTU avae apendavyo...we unamuangalia MTU kavaa Nini huna kazi ya kufanya..

Yale yale,ikija mada za mashoga unapinga kwa nguvu mpaka mishipa ya mavi inalegea. Wakati ni huru wake yeye.

Hivi kumuonesha mfereji wa maji machafu na makalio mwanaume mwenzio ni huru?
 
Kwanza, niupongeze kwa dhati uongozi huo wa kijiji. Ni nadra siku hizi viongozi wakikerwa na shida ktk jamii wanachukua hatua, wengi ni kulaumu na kulalama tu!

Kisheria mamlaka waliyonayo viongozi wa vijiji inawaruhusu kutunga sheria ndogondogo kusimamia utawala wao. Hili wala siyo la kwanza, Manispaa ya Moshi ukitupa taka faini papo kwa hapo, ila Temeke popote ni dampo!! Miji yote inaiga Moshi, kwa hiyo vijiji vingine vikiiga sii baya. Kama unawaona Arusha wamekaza sana, nenda Zenji na kipedo au kata K. ..... Sitaki kuwa shahidi mie!!

Kuna mtu humu anauliza nafasi ya wakuu wa dini kuhukumu, eti wao hawana dhambi? Kwani nani alikuambia hakimu ni mtakatifu, si naye anahukumu? Tena wangine kifo na wananyongwa?

Ukienda kwa watu, uliza kwanza!!

Unatoa mifano ya vitu ambavyo havifanani kabisa! Kuhadhibu wachafuzi wa mazingira na mvaa min skirt ni vitu viwili tofauti. Hakuna sehemu yoyote ktk Tanzania unaruhusiwa kutupa hovyo uchafu. Kama hatua hazichukuliwi maeneo mengine ni udhaifu wa viongozi na wananchi wa eneo hilo!

Tanzania siyo nchi ya kidini ama mila za jadi. Watu mnaojiita waumini wa dini mmegeuka kero kwa makelele usiku na mchana mbona hamkemei huo upuuzi?? Hivi lubega ina tofauti gani na hawa wa milegezo na mini skirt?

Ni standard gani mtasema hii ni skirt na hii min skirt? Wengine ndizo nguo za kazi. Na je mtoto wa tajiri/kiongozi hapo kijijini akivaa nani atamgusa?? Kama siyo kuwadhalilisha wasichana na wanawake masikini?? Akitembelea Mzungu/Mtalii amevaa hivyo wana ubavu wa kumchapa viboko? Taifa halipaswi kuruhusu watu wenye mawazo ya kijima kuingilia uhuru wa mtu binafsi! Kama unachukia mavazi hayo walee wanao ktk malezi yaliyo bora siyo kuangalia mtoto wa jirani yako anavaaje!
 
MKUTANO Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru umeazimia kuwachapa viboko vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.

Mkutano huo umepitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima kijijini Olgilai limefikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa nguo zisizo na heshima.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24 mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza:

“Viongozi wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote wakubwa kwa wadogo.”

Katika barua yake ambayo MTANZANIA inayo nakala yake Mwenyekiti huyo alisema kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hili na kuamuru lianze kutumiwa Januari 24 mwaka huu.

Aliyataja maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko.

Jingine ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama.

“Vijana wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa viroba, uchezaji kamari na karata.

“Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani watashughulikiwa,” alisema Boazi.

Alisema Mkutano Mkuu wa Kijiji ulijiridhisha kuwa matendo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa nidhamu kijijini hapo na maeneo mengine.

Mtanzania 30/01/2014

Nini maoni yako?

UAMSHO!!! Ritz
 
Last edited by a moderator:
MI Ngoja nisubiri utekelezaji kama utawezekana maana mashirika ya kimataifa na wanaharakati njaa hawatachelewa kuingilia, Kuenzi tamaduni zetu(ukeketaji,kuoa wanawake wengi, kuzaa watoto wengi,kukatwa ulimi kimila) tunaambiwa ni mila potofu kuvaa vichupi na suruali zilizo bana kuacha nusu matiti nje kwa wanada, wanaume kusuka, kuvaa hereni kuoana jinsia moja tunaambiwa mambo ya kisasa (kwenda na wakati) haya bwana.
 
Hii gharama ya kuwachapa viboko itafadhiliwa na nani? i mean vijana wachapwe bakora kwa hisani ya watu wa wapi?
 
kaz ipo cshangai nyie mnaotetea mlegezo kwani hata wanaotetea mashoga wapo na wanaona mashoga ni watu wa kawaida
 
Hii kitu nzuri Sana Taifa letu litarudi mahali yake. Nao viongozi mafisadi nao watachapwa tu 😂

Back
Top Bottom