Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Mkuu umenena kweli. Maana sio kila atakayekuwa hapo kijijini ni mkazi wa kijiji hicho. Na hata kama ni mkazi wa kijiji hicho, sidhani kama ni sahihi kila kijiji kuwa na sheria yake (hasa zinazohusiana na uhuru wa mtu mmoja mmoja).
Tunaweza tukaishangilia hii, lakini kesho tukasikia kijiji kingine wakasema ni marufuku kusuka nywele, wengine ni marufuku kupaka kucha rangi, wengine ni marufuku kusikiliza miziki ya aina fulani nk.

Kweli kabisa mkuu wangu. Hakuna watu wavunjaji haki za binadamu ktk maeneo ya vijijini na watu masikini kama vikundi haramu vya aina hiyo vikijiita watetezi wa mila ama dini!
 
Mafisadi na wala rushwa wenyewe waendelee kutanua.
nchi hii we acha tu
 
Huo ni upuuzi kwani mi nikivaa mlegezo we unakuuma nini afu viongozi wa dini wanahukumu kwani wao wamekua Mungu au hawana dhambi hayo ndio matatizo ya kukosa kazi unabaki kufuatilia tu vijana
 
nchi ikiachwa watu wakaset standard zao wanazo dhania wao ndiyo maadili ktk jamii yao kutaibuka makundi haramu yanayo dhalilisha wanawake kwa visingizio vya dini na mila.

viongozi wa eneo husika waingilie kati mara moja kabla hali ya mambo haijaharibika. maoni yangu ni kutoka ktk historia ambako makundi haramu yanayo jiita ama watetezi wa dini ama mila yaliibuka na kuvunja kwa kiwango kikubwa haki za binadamu. ningesikia wamepiga marufuku wasiende ktk nyumba za ibada wamevaa vimini na milegezo ningeelewa lakini sivinginevyo.
sometimes ubabe unasaidia kama mtu hataki diplomasia
 
Kweli mkuu. Tatizo la serikali yetu itaacha mpaka watu wamejeruhiwa au kuuawa hapo ndipo itakurupuka na kuanza kuunda tume. Mambo haya ni hatari sana. Huko kupiga ni kwa kiwango gani na ni nani atakayekuwa anapiga? Je wapita njia nao watahusika? wageni je ambao sio wanakijiji hicho? Haya yatakuwa kama yale yanayofanywa na sungu sungu kanda ya ziwa ambao ni kama polisi na mahakama. Vyombo vya habari ambavyo serikali ndio adui yake mkuu ambapo huvifungia mara kwa mara vimetimiza wajibu wake kwa kuipasha jamii kuhusu maamuzi hayo hatari. Sasa siji serikali itaamka lini.
 
Mi nafikiri hayo maamuzi ni magumu kutekeleza sketi fupi ni ipi? Nguo za kubana ni zipi na nani ana wajibu wa kuchapa wengine.

Mtu mmoja aliniambia "A mini skirt is short enough to arouse interest but long enough to cover what it covers"
 
Ujinga unapofikia hatua ya mwisho matokeo yake ni maamuzi ya kissenge kama haya!

Kukusaidia ni kuwa umeleweshwa na kikombe cha ukahaba na hivyo umeingiwa na wazimu wa uasherati: SOMA UFUNUO WA YOHANA 17 kutoka katika Biblia Takatifu.
 
Kukusaidia ni kuwa umeleweshwa na kikombe cha ukahaba na hivyo umeingiwa na wazimu wa uasherati: SOMA UFUNUO WA YOHANA 17 kutoka katika Biblia Takatifu.

Nawewe umedanganywa na bikira maria yule mliyeipaiza mbinguni?
Unajiganya unajuaaaaa dini kumbe hewa tuu.
Jadili hoja mkuu,sio taarabu.
 
sometimes ubabe unasaidia kama mtu hataki diplomasia

hili jambo wala halihitaji ubabe,hapa ni malezi ! na usidhani mimi naunga mkono mavazi yasiyo na staha bali napinga kitendo cha watu wa kila eneo kukaa na kuset standard zao! sheria za nchi zifuatwe!

na bahati nzuri nimeishi arusha kwa miaka kadhaa na hicho kijiji nakifahamu,ni jamii fulani ambayo kwa viwango vya kwenda shule bado wanakabiliwa na ujinga.
 
Nawewe umedanganywa na bikira maria yule mliyeipaiza mbinguni?
Unajiganya unajuaaaaa dini kumbe hewa tuu.
Jadili hoja mkuu,sio taarabu.

huna sababu ya kukejeli dini/dhehebu la watu wengine kwasababu tu umetofautiana kwa hoja na mtu mmoja!
 
Mimi huwa nashangaa sana, mwanaume unavaa mlegezo, makalio yote nje,, Je unataka upumuliwe kisogoni? ujinga mtupu!
 
huna sababu ya kukejeli dini/dhehebu la watu wengine kwasababu tu umetofautiana kwa hoja na mtu mmoja!

Unadandia hoja bila kuangalia chanzo.
Ref.
Post iliyosema hivo,juu yake kuna maelezo gani.
Ahsante kwa maoni yako ya kukurupuka,sitayafanyia kazi!
 
Hao viongozi wa kanisa wamekuwa Mungu mpaka wahukumu? Watahukumu matendo ya nje je ya mioyoni? UKRISTO ni kuonya kwa upole na amani hukumu ni kazi ya MUNGU.Habari za al-shabab hizo nendeni mkaishi somalia nyambaf nyie!

Isokuwasha hujailamba
 
Kuingilia Uhuru Wa MTU sio issue...kila MTU avae apendavyo...we unamuangalia MTU kavaa Nini huna kazi ya kufanya..
 
Jamani watanzani tuna kwendawapi kijiji kimebuni jambo lamaana na lakuiga kwan sio utamaduni wetu kutembea uchi hayo tueaachie wazungu kwani hata miili yao haivutii mswahili akitembea nusu uchi ni shida tumuogope mungu ktk kulea taifa hili
 
Hivi utamaduni wetu ni upi?
Ni huu?
Dada zetu warudi huko?
 
Attachments

  • 1391086104126.jpg
    1391086104126.jpg
    66.8 KB · Views: 211
mimi naona tungeanza na wanaoendesha bodaboda kwa fujo kwanza tukifanikiwa hili ndio tuendelee na hayo mengine.
 
This is against human rights how can you decide for others we have to let people live their lives YOLO
 
Mahakama za kiraia ziliifanya somalia isitawalike, serikali iwe makini. Anyway, nani ana-define kimini, mlegezo na skintight vinginevyo tujiandae kwa madudu ya Operation Tokomeza.

kuna mambo mengine hayahitaji definition yapo wazi ukweli ni kwamba adhabu hiyo iwepo ila iwe na kiasi
 
Back
Top Bottom