Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Wavaa mlegezo, vimini kuchapwa viboko

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,266
MKUTANO Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru umeazimia kuwachapa viboko vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.

Mkutano huo umepitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima kijijini Olgilai limefikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa nguo zisizo na heshima.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24 mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza:

“Viongozi wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote wakubwa kwa wadogo.”

Katika barua yake ambayo MTANZANIA inayo nakala yake Mwenyekiti huyo alisema kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hili na kuamuru lianze kutumiwa Januari 24 mwaka huu.

Aliyataja maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko.

Jingine ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama.

“Vijana wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa viroba, uchezaji kamari na karata.

“Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani watashughulikiwa,” alisema Boazi.

Alisema Mkutano Mkuu wa Kijiji ulijiridhisha kuwa matendo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa nidhamu kijijini hapo na maeneo mengine.

Mtanzania 30/01/2014

Nini maoni yako?
 
hata kijijini kwetu pombe imepigwa STOP... Wanawake hawaruhusiwi kuvaa trouser na sketi fupi...Haya yapo sana Maasai villages..
 
Jamani jamani nadhani tunaelekea ama tumefika kule maandiko yaliposema ........

Nilimuona dada mmoja jana kavaa suruali, ukimuona kwa umbali kidogo kama zaidi ya mita15 utasema yuko uchi kabisa. Suruali inambana na yeye nyuma ana mzigo mkubw sana. Ni aibu sana kukutana kwa kweli mbele ya uma.
Alikuwa akikatiza mtaa wa Ohio muda wa saa 1 asubuhi akaingia eneo la jengo linalotazamana na sukari house huku akiwaacha watu midomo wazi. Huyo dada kimtazamo wangu alikuwa uchi 95%
 
Ujinga unapofikia hatua ya mwisho matokeo yake ni maamuzi ya kissenge kama haya!
 
Hao viongozi wa kanisa wamekuwa Mungu mpaka wahukumu? Watahukumu matendo ya nje je ya mioyoni? UKRISTO ni kuonya kwa upole na amani hukumu ni kazi ya MUNGU.Habari za al-shabab hizo nendeni mkaishi somalia nyambaf nyie!
 
me sioni kama ni jambo jema ... hapao amana uhuru.....

huko kijijini wangetumia nguvu zao kuwachapa wabunge na viongozi wote wezi na mafisadi.....
 
Hao viongozi wa kanisa wamekuwa Mungu mpaka wahukumu? Watahukumu matendo ya nje je ya mioyoni? UKRISTO ni kuonya kwa upole na amani hukumu ni kazi ya MUNGU.Habari za al-shabab hizo nendeni mkaishi somalia nyambaf nyie!
kabisa yani wanaacha hao wezi na mafisadi wanapmbana na watu wano tumia ujana wao vizuri
 
Mi nafikiri hayo maamuzi ni magumu kutekeleza sketi fupi ni ipi? Nguo za kubana ni zipi na nani ana wajibu wa kuchapa wengine.
 
Hiyo kitu ingekuja na huku mijini. Safi sana tumechoka kuona mat.ko ya watu wazima njenje. Nidhamu hakuna kabisa sio vibinti wala mitoto nya kiume. Viboko tu ndo dawa saivi. WAPIGWE TU....
 
Vinauzi sana hivi vijank hata enzi yetu hatukupiga milegezo mikubwa kiasi cha leo wachapwe tu ndio dawa yao
 
so good...........ni mfano wa kuigwa!

nchi ikiachwa watu wakaset standard zao wanazo dhania wao ndiyo maadili ktk jamii yao kutaibuka makundi haramu yanayo dhalilisha wanawake kwa visingizio vya dini na mila.

viongozi wa eneo husika waingilie kati mara moja kabla hali ya mambo haijaharibika. maoni yangu ni kutoka ktk historia ambako makundi haramu yanayo jiita ama watetezi wa dini ama mila yaliibuka na kuvunja kwa kiwango kikubwa haki za binadamu. ningesikia wamepiga marufuku wasiende ktk nyumba za ibada wamevaa vimini na milegezo ningeelewa lakini sivinginevyo.
 
Mh!!!

Kila kijiji kikijitungia sheria zake, hii nchi itakalika kweli?
 
nchi ikiachwa watu wakaset standard zao wanazo dhania wao ndiyo maadili ktk jamii yao kutaibuka makundi haramu yanayo dhalilisha wanawake kwa visingizio vya dini na mila.

viongozi wa eneo husika waingilie kati mara moja kabla hali ya mambo haijaharibika. maoni yangu ni kutoka ktk historia ambako makundi haramu yanayo jiita ama watetezi wa dini ama mila yaliibuka na kuvunja kwa kiwango kikubwa haki za binadamu. ningesikia wamepiga marufuku wasiende ktk nyumba za ibada wamevaa vimini na milegezo ningeelewa lakini sivinginevyo.

Mkuu umenena kweli. Maana sio kila atakayekuwa hapo kijijini ni mkazi wa kijiji hicho. Na hata kama ni mkazi wa kijiji hicho, sidhani kama ni sahihi kila kijiji kuwa na sheria yake (hasa zinazohusiana na uhuru wa mtu mmoja mmoja).
Tunaweza tukaishangilia hii, lakini kesho tukasikia kijiji kingine wakasema ni marufuku kusuka nywele, wengine ni marufuku kupaka kucha rangi, wengine ni marufuku kusikiliza miziki ya aina fulani nk.
 
Back
Top Bottom