Umakini wa kukusanya kodi
unaofanywa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), umeanza
kudhoofisha biashara katika
baadhi ya maduka ya bidhaa
mbalimbali, ikiwamo simu eneo la
Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Gazeti hili lilifika katika maduka ya
simu ya Mtaa wa Msimbazi na
Kariakoo na kukuta baadhi yakiwa
na simu kidogo wakati zile za
gharama kubwa zikiwa chache.
Baadhi ya wauzaji walidai kodi
imechangia uhaba huo, kwa kuwa
kila kinachoingizwa nchini kwa
sasa kinalipiwa.
Mmoja wa wafanyabiashara hao,
Agban Singh alisema ni bora
kuagiza simu za bei ya kawaida
kuliko za gharama kwa sababu
wanunuzi hakuna na kodi ni
asilimia 100.
“Unajua ni tofauti na zamani. Hivi
sasa hakuna mzigo unaopita bila
kukatwa (kodi) kitu ambacho
kinachangia kuwapo kwa mizigo
michache na ya kawaida,” alisema.
Sufiani Khamis aliyekuwa
anachukua simu na kuzitembeza
kwenye baa na maeneo ya
starehe, alisema ameacha kufanya
biashara hiyo, badala yake
anashinda dukani kwa tajiri yake
wakiuza zilizopo kwa sababu
mzigo uliopo ni mdogo.
“Si unaona hata mali zilizopo siyo
za gharama ni za kawaida, kuagiza
simu halisi hivi sasa siyo kitu
rahisi, ukileta mzigo uwe
umejipanga. Hakuna ujanjaujanja,
sijui kama tutaendelea kuagiza
mzigo wa maana, ”alisema.
Akbar Yunus alisema
wafanyabiashara wengi wadogo
walikuwa wanatamba kutokana na
kushirikiana na wafanyabiashara
wakubwa kuagiza mizigo
‘kimtindo’, lakini sasa kila mtu
anayeagiza wa kwake anatakiwa
alipie kodi halisi kulingana na
mzigo.
“Wengi hawakuwa na mtaji wa
kutosha, lakini walikuwapo,”
alisema. Yunus.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu
kwa Walipakodi wa TRA, Richard
Kayombo alisema hawajamkataza
mfanyabiashara yeyote kuagiza
mzigo na wala hawatozi kodi kwa
kukomoa, bali kwa kufuata sheria
zilizopo.
“Mfanyabiashara anayefanya
shughuli zake kwa usahihi hana
haja ya kuogopa, ”alisema
Kayombo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.