Naomba nikuulize wewe Lyambasa, kabla ya kuishi naye , ulimchunguza ukamfahamu alivyo? je ulituma wazzee kwenda kuchunguza ukoo wao ukoje na wana tabia gani? mimi nafikiri ndiyo maana ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu hatufuati taratibu zilizokuwepo, mtu unajiamulia tu unakwenda kuoa, ukishauriwa hutaki, Leo yanawakuta mnarudi kulalamika, Yaani wewe ni kama kaka yangu alishauriwa na wazee kuwa anayetaka kuoa si mke ankang'ang'ania siku hizi halali ndani kwake kwa sababu ya vurugu, imefika mahali kaamua kurudi kwa wazazi home ndipo anapata kupumzika.
kwa hiyo nakuomba fanya uchunguzi ufahamu tabia yake, ukoo wao, halafu itakubidi ufanye maamuzi magumu ya kumuacha na kutafuta mke na umwambie kuwa una watoto na yeye ndiye anatakiwa kuwalea hao watoto.