Lyambasa
Senior Member
- Sep 24, 2013
- 153
- 43
Wana MMU naombeni ushauri wenu.Nimekuwa nikiishi na dada mmoja kama mke wangu ambapo tumebahatika kupata watoto wawili.Wakati tunoana alikuwa na mtoto wake ambaye alizaa na mwanaume mwingine ambaye inasemekana aliachana naye.Binafsi nilihisi kuwa huenda dada huyu kwa kuwa sasa ni mtu mzima maisha ya ndoa yetu yangeenda vizuri.Lakini sasa ni vurugu mtindo mmoja na anichafua kila kona mimi pamoja na familia yangu.Kili mgeni mwanamke ni hawala yangu mpaka ndugu zangu na zake.Kila akinikosea anakimbilia kwa mchungaji wa church yangu,hujui kusema ahsante wala samahani na mbaya zaidi sasa anamtangaza mama yangu kuwa ni mchawi.Nilimpeleka kwao kwa muda nikitegemea mama mkwe atamshauri lakini kinyume chake anaona namuonea mwanaye.Wamenifanyia visa ambapo imefika hatua ya kushindwa kujua hatima ya wanangu ambao ni wadogo sana,wakati huo huo nina mgogoro kazini. Nifanyeje waungwana