happiness win
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 2,461
- 1,394
Ni wanaume wachache sana wenye moyo mgumu mbele ya wanawake. Ukiona mwanamke anapata shida kwa mume wake, ni sababu ya VIBURI, GUBU na KUTOJIHESHIMU kwa wanawake hao.
Virukanjia wengi sana wamejibadili majina siku hizi wote wanajiita wake, lkn wamepinda na ndio wanaishia kwenye vibano. Mwanamke anayejitambua na kuzijua silaha zake siku zote atapendwa na mumewe. Ukitanua mbavu lazima uchapike
Tunaelewa kwamba mke ametoka katika ubavu wa mume. Hakutoka katika nyayo ili adharauliwe na kukandamizwa wala hakutoka katika kichwa ili mwanamume ajisifu kuwa yeye ana akili sana; bali ametoka ubavuni ili akumbatiwe na kulindwa, kumbuka ametoka ubavu wa kushoto ulio karibu na moyo ili apendwe, aheshimiwe na kuthaminiwa.
Kwa kuwa ubavu haujanyooka sawa sawa mke pia ana mapungufu, lakini asinyooshwe kwa nguvu atavunjika, akanywe kwa upole na upendo naye atasikia.
Mke ana ana akili, huruma, hisia na akifanyiwa yote hayo huwa kitu chema, tofauti na hivyo unamharibu na kuondoa lengo la Mungu kukuumbia msaidizi. Kumbuka mwanamke akiharibika hutaweza kumrudisha katika hali halisi aliyoumbwa nayo utaishia kuona mwanamke ni kiumbe hatari kisichostahili kuishi duniani.
Mambo haya yote yanaanza toka mwanamke anapozaliwa, apendwe, alindwe na atunzwe. Wapende dada zako/binti zako hadi watakapokuwa wake za watu na hadi kifo.
Umenena vyema sana happiness win. Lakini hiyo isiwe sababu ya baadhi yao ku-misbehave, wanapaswa nao kuheshimu, kupenda nk. Upendo uwe niwa pande zote mbili vinginevyo hali bado itakuwa mbaya kwenye mahusiano. Ila ujumbe tumeupokea.
Sasa unamaanisha demu au ndo nini sasa!
Dada, binti na wanawake ni vitu tafauti!
Usinchanganye.
Adam mwenyewe alipobananishwa si akaropoka
"si ni huyu mwanamke ulionipa!"
Tunaelewa kwamba mke ametoka katika ubavu wa mume. Hakutoka katika nyayo ili adharauliwe na kukandamizwa wala hakutoka katika kichwa ili mwanamume ajisifu kuwa yeye ana akili sana; bali ametoka ubavuni ili akumbatiwe na kulindwa, kumbuka ametoka ubavu wa kushoto ulio karibu na moyo ili apendwe, aheshimiwe na kuthaminiwa.
Kwa kuwa ubavu haujanyooka sawa sawa mke pia ana mapungufu, lakini asinyooshwe kwa nguvu atavunjika, akanywe kwa upole na upendo naye atasikia.
Mke ana ana akili, huruma, hisia na akifanyiwa yote hayo huwa kitu chema, tofauti na hivyo unamharibu na kuondoa lengo la Mungu kukuumbia msaidizi. Kumbuka mwanamke akiharibika hutaweza kumrudisha katika hali halisi aliyoumbwa nayo utaishia kuona mwanamke ni kiumbe hatari kisichostahili kuishi duniani.
Mambo haya yote yanaanza toka mwanamke anapozaliwa, apendwe, alindwe na atunzwe. Wapende dada zako/binti zako hadi watakapokuwa wake za watu na hadi kifo.
Iko poa, ila umesahau kitu kimoja kwa wanawake, ambacho ni "wanawake watiini waume zenu".
Tabia zote mbaya ulizozitaja zinatokana na malezi wanayoyapata wanawake toka siku ya kwanza kuingia duniani. Ile anazaliwa tu Baba anasema "umezaa toto la kike, shida tupu", malezi yatakayoendelea baada ya hapo si ya upendo tena, unadhani nini kitatokea... ndio hizo tabia. Ndio maana nikasema Wababa, wakaka, wapendeni wanawake, yaani kuanzia dada zenu hadi wake zenu. Wanawake ni viumbe vya kulelewa kwa tahadhari.
nimeongelea wanawake, nikasema wanapaswa kupewa upendo toka wakiwa tumboni. Hivyo mwanao wa kike, dada yako, na baadae mkeo au demu wako kama unavyoita.
Hivi mwanamke anayemjibu hovyo mume wake anakuwa alifundishwa na baba yake eti? Yapo mambo ambayo ni zao la ukuaji, lakini mengi wanafundisha wenyewe ukubwani.
Hapa JF kumejaa manungayembe yanataka kuolewa, at the same time ndoa imegeuka kuwa 'a business of equal shares' as if kuna kitu tunashindania. Hakuna cha kuwataka hawa wafanye hivi, wala wale wafanye vile, tukiufuata mpango wa Mungu hakuna wa kuijutia ndoa.
Asante kwa kupokea ujumbe, wapende wanao wote na dada zako (ila hapa naongelea wa kike). Toka tumboni hadi wanazaliwa na kukua hadi kuolewa kama wangelelewa kwa upendo nao wangejifunza kupenda, kuheshimu na kuthamini wengine.
sema ni wachache wajuayo haya yoote!!!
Thanks, Wanangu wameshaolewa tayari sasa hivi nalea vijukuu.
Ni kweli Biblia inasema hivyo. Lakini Utii kwa mtu asiyekupenda unakuwa na walakini tena unakuwa wa kuigiza tu kwa muda mwishoni dharau huchukuwa nafasi. Ukisoma vizuri Neno hilo lilianza na ENYI WANAUME WAPENDENI WAKE ZENU...
sema ni wachache wajuayo haya yoote!!!