happiness win
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 2,461
- 1,394
Tunaelewa kwamba mke ametoka katika ubavu wa mume. Hakutoka katika nyayo ili adharauliwe na kukandamizwa wala hakutoka katika kichwa ili mwanamume ajisifu kuwa yeye ana akili sana; bali ametoka ubavuni ili akumbatiwe na kulindwa, kumbuka ametoka ubavu wa kushoto ulio karibu na moyo ili apendwe, aheshimiwe na kuthaminiwa.
Kwa kuwa ubavu haujanyooka sawa sawa mke pia ana mapungufu, lakini asinyooshwe kwa nguvu atavunjika, akanywe kwa upole na upendo naye atasikia.
Mke ana ana akili, huruma, hisia na akifanyiwa yote hayo huwa kitu chema, tofauti na hivyo unamharibu na kuondoa lengo la Mungu kukuumbia msaidizi. Kumbuka mwanamke akiharibika hutaweza kumrudisha katika hali halisi aliyoumbwa nayo utaishia kuona mwanamke ni kiumbe hatari kisichostahili kuishi duniani.
Mambo haya yote yanaanza toka mwanamke anapozaliwa, apendwe, alindwe na atunzwe. Wapende dada zako/binti zako hadi watakapokuwa wake za watu na hadi kifo.