measkron
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 3,782
- 2,406
Wana jf naomba tujadili hapa kwani napata uchungu kuona hata taaluma inaendeshwa kisiasa, kusoma uuguzi miaka 2 source ITV news jana usiku, kutapunguza vifo vya kina mama? Nimejaribu kufanya mazungumzo na baadhi ya wauguzi kilimanjaro,Arusha na Tanga wengi wao wakisikitishwa na uamuzi huo, vyama vya wauguzi TANA, TAMA kama mnapita humu jamvini tunaomba mtoe maoni yenu. Pili ni mavazi ya wauguzi mkikumbuka walikuwa wanavaa gouns na vibandiko kichwani, nywele zimebanwa ama kusuka vizuri, vyote vimeondoka siku hizi, muuguzi unamkuta amesuka rasta zinafunika uso, maadali yako wapi? Siku kama ya leo ni sikukuu ya wauguzi duniani tunaomba wajadili mambo yenye tija kwa taifa ikiwemo kuangalia hjo usomaji wa uuguzi kwa miaka miwili sijui watasoma Medisurgical,General nursing, Community nursing, Midwefery kwa miaka miwili na kumaliza,.......