Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 373,018
- 864,149
Karama na vipawa ni tunu mtu atunukiwazo bure na Mungu, hadai hata senti moja na si wote wanajaaliwa kuvipata, bali Mungu huwapa wale aliowachagua ili wakautumikie ulimwengu kwa niaba yake karama na vipawa si vitu unaweza kwenda shule ukavisomea na kufaulu kwanza hakuna shule za namna hiyo Mungu anatambua uwepo na kazi zifanywazo na hawa manabii na mitume, ni yeye mwenyewe ndio kawakirimia vipawa na karama ili wakautumikie ulimwengu,kawapa bure kwenye maandiko matakatifu kuna mstari unasema 'nimewapa bure toeni bure' kawapa vipawa na karama za kuhubiri, kuponya , kuhuisha, kufufua na kutenda miujiza mingi.
Kawapa bure kabisa.Lakini ni Mungu huyu huyu anayetuasa kuwa tusiwaamini hawa pamoja na kufanya miujuza yote hiyo tena kwa jina lake! Unatambua ni kwanini?Ni kwasababu si watumishi waaminifu ni watumishi wezi waliopewa bure ili wakauponye ulimwengu lakini wao wanatoza fedha na kujilimbikizia mali na utajiri huku wakiishi maisha ya starehe na anasa nyingi Mungu anaona na hesabu ya matendo yao itakuwa siku ya kiama kile kinachopatikana kwenye huduma wazitoazo walipaswa wakirudishe kwa Mungu kwa njia kusaidia ulimwengu kwa kujenga vituo vya watoto yatima wajane na wasiokuwa na makazi, kwa kujenga vituo vya afya na hospitali kwa kusaidia kwenye nyanja za elimu lishe na upatanishi, nk.
Lakini ndugu zangu hawa wanatenda tofauti wanatanua kwa kushindana kumiliki mali nyingi wanashindana kuvaa wanashindana kuendesha magari ya kifahari zikiwemo ndege na vyombo vya majini wanashindana kwa kila kitu huu ni wizi huku ni kukosa uaminifu.Mungu anaona na anaona kweli jinsi waumini maskini wanavyozidi kukamuliwa kila kukicha huku akaunti za manabii zikizidi kuvimbiwa mihela.
GOD IS WATCHING!