Watumishi waliohamishwa tar 26 March na hawajapata vibali tukutane hapa

Fasouls

JF-Expert Member
Jun 24, 2011
939
316
Habari zenu ndugu,

Mpaka sasa inapita mwezi mmoja na wiki kadhaa ila vibali hakuna ingawa kuna kwa baadhi ya halmashauri wamepata.

Kwa wale ambao bado tufanyaje mana kwangu mimi nilipata uhamisho kwa kubadilishana na niliebadilishana nae nipo nae huku, tena naishi nae kabisa kwa maana ya kwamba mimi nikiondoka yeye nimwachie nyumba.

Sasa muda unaenda vibali hakuna na morali ya kazi imepungua kabisa kitu kinachoathiri utendaji wa kazi, ukiwapigia utumishi wanasema wametuma ukienda halmshauri wanasema hakuna sasa haieleweki kua nini tatizo au vibali vimefichwa? Au kukwama wapi?
 
Back
Top Bottom