Watumishi waliofoji umri hawana tofauti na waliofoji vyeti

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Tusubirie matokeo ya uhakiki wa NIDA kwa watumishi wa umma.

Kuna kila dalili ya kubainika idadi kubwa ya watumishi wenye umri tata. Hawa kwa makusudi walifanya udanganyifu kwa kughushi umri.Madhara ya kughushi umri ni makubwa kama ya kughushi vyeti.

Watumishi hawa wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu kwa kumuongopea mwajiri aidha wastaafu haraka au wachelewe kustaafu.

Hivyo natoa rai kwa serikali iwachukulie hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutumbuliwa kama wa vyeti feki.

Nina imani serikali ya Magufuli haitowaacha salama.

Ikumbukwe udanganyifu HAUMWACHI MTU SALAMA.
 
NIDA wanauwezo wa kutambua umri wa mtu? Hujui NIDA ili upate kitàmbulisho kunahtajika na cheti cha kuzaliwa? Kwa akili yako unadhan cheti cha kuzaliwa cha NIDA kina utofauti na cheti cha kuzaliwa cha mtu aliepo ktk utumish wa umma,!?
 
Kama hujui miaka yako ufanyaje? Serikali haifanyi kaz kama hyo ni upotevu rasilimali kama makinikia kwa kufatilia hili, ikumbkwe mtu haajiriwi kwa cheti cha kuzaliwa, kila kitu ni taaluma, usiwe nakinyongo kama umetumbuliwa na vyeti fake,

Note; Kama mhanga urud shule kama umeptiwa na vyeti fake! Kusubr uhakiki wa umri ili nafsi yake ifurah ni umaskn!
 
mambo y
Tusubirie matokeo ya uhakiki wa NIDA kwa watumishi wa umma.

Kuna kila dalili ya kubainika idadi kubwa ya watumishi wenye umri tata. Hawa kwa makusudi walifanya udanganyifu kwa kughushi umri.Madhara ya kughushi umri ni makubwa kama ya kughushi vyeti.

Watumishi hawa wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu kwa kumuongopea mwajiri aidha wastaafu haraka au wachelewe kustaafu.

Hivyo natoa rai kwa serikali iwachukulie hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutumbuliwa kama wa vyeti feki.

Nina imani serikali ya Magufuli haitowaacha salama.

Ikumbukwe udanganyifu HAUMWACHI MTU SALAMA.

hapo itakuwa maajabu sana , kwani umri wa mtu ni utashi wa wazazi wake, na pengine umri alioandikisha mtu ni wa kukadilia kutokana na mahali alipo zaliwa , kuna wengine wameokotwa na kulelewa katika vituo vya kulelea yatima, wakakua na kusomeshwa, sasa hebu tuambiane kweli bila kumumunya maneno, hawa wanakosa gani? kinachotakiwa siyo hicho msipotoshe umma. suala la umri siyo masihala, iwapo tu wazee wetu wanakadiliwa umri wao wakati wa sensa, sasa kama ni hivyo, wana kwepa nini na kupata nini? au kwa sababu tu watumishi wa umma wamekaliwa kooni?
 
Tusubirie matokeo ya uhakiki wa NIDA kwa watumishi wa umma.

Kuna kila dalili ya kubainika idadi kubwa ya watumishi wenye umri tata. Hawa kwa makusudi walifanya udanganyifu kwa kughushi umri.Madhara ya kughushi umri ni makubwa kama ya kughushi vyeti.

Watumishi hawa wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu kwa kumuongopea mwajiri aidha wastaafu haraka au wachelewe kustaafu.

Hivyo natoa rai kwa serikali iwachukulie hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutumbuliwa kama wa vyeti feki.

Nina imani serikali ya Magufuli haitowaacha salama.

Ikumbukwe udanganyifu HAUMWACHI MTU SALAMA.

suala lingine ambalo unatakiwa kulifahamu, je, hizo taarifa umezitoa katika chanzo kipi mkuu? na je, unayafahamu makusudio ya NIDA?
 
na je, NIDA ni kwa ajili ya watumishi wa umaa tu? mimi nadhani iko kwa ajili ya kuandaa vitambulisho vya taifa, na kinachofanyikoa katika uhakiki wa sasa ni kuhakikisha jina la kwenye kitambulisho cha kazi, salary slip na kwenye kitambulisho cha NIDA yanaendana sawia. kuna jamaa yeye aliambiwa alipie gharama za kutengenezewa kitambulisho kingine baada ya kuona kuwa jina la kwenye kitambulisho linatofautiana na mengine, kwa nini alilipia? kwa sababu makosa aliyafanya mwenyewe-ila wangekuwa wao, basi wangemtengenezea kitambulisho kingine bila malipo. sasa ya umri yametoka wapi? kwani wana CA14?
 
Back
Top Bottom