Watumishi wa umma ni ATM kwa ndugu zao na majirani kama mlivyo nyinyi wabunge

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,651
Watumishi wa umma ni walipa kodi namba 1 hapa Tanzania kuliko mtumishi yoyote yule. Mtumishi wa umma anafanya kazi kubwa kuliko mbunge anaye kwenda kusinzia na kutoa kejeli bungeni. Watumishi wa umma wamesoma na wanaelimu kubwa kuliko 90% ya wabunge.

Mshahara wa mtumishi wa umma ni mdogo kuliko wa mbunge na bado mtumishi huyo anakuwa na msurulu wa wategemezi wanaokwenda kumuomba misaada. Hivyo kama ni suala la kuwa ATM, watumishi serikalini ndiyo ATM nambari wani.

Nyie wabunge msijifanye ndiyo mnajuwa sana kusaidia watu. Lipeni kodi kama vile ambavyo mtumishi wa serikali anavyolipa. Ubinafsi, uchoyo na ulafi utawaangamiza nyie wabunge.

LIPENI KODI TUIJENGE TANZANIA YETU.
 
Mkuu unaweza ukawa na point kubwa sana, hapa hoja ni working class, haijalish ni private au public, hakuna kisingizio cha hovyo nilichowahi kusikia kama hiki cha kuwa ATM kutoka kwa mbunge mwenye privilege zote za diplomats
Ipo haja ya kuwabana zaidi, wengi sio kusinzia tu lakini hata hoja wanazojenga ni urojo wa kutisha, hivi kuna haja gani kuwa na watu wa aina hii ambao hata hawasomi wanachotakiwa kuchangia au kuzungumza? jamii ianze kuwakataa wabunge wa hovyo namna hii( kwao maslahi tu na wala si kwa wananchi waliowachagua)
 
Kweli Mkuu, unakuta mtumishi wa umma labda ndio unakuta kwao ndio wa kwanza kusoma na kupata kazi kwahiyo unakuta kila mtu kwao anamtegemea yeye,mara ada kwa wadogo zake, mara kutunza familia yaani kila kitu anakuwa ameachiwa yeye afu mshahara wenyewe ndio huo ambao serikali imekata kodi kibao.Jamani waheshimiwa wabunge tulipeni tu kodi haina jinsi wenyewe wanasema "Kulipa kodi ni uzalendo"
 
Hakuna namna nao wakatwe tuu kama watumish wanavyolipa kodi na wanavyokatwa kwenye mafao, kila mtanzania alipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu
 
Kweli Mkuu, unakuta mtumishi wa umma labda ndio unakuta kwao ndio wa kwanza kusoma na kupata kazi kwahiyo unakuta kila mtu kwao anamtegemea yeye,mara ada kwa wadogo zake, mara kutunza familia yaani kila kitu anakuwa ameachiwa yeye afu mshahara wenyewe ndio huo ambao serikali imekata kodi kibao.Jamani waheshimiwa wabunge tulipeni tu kodi haina jinsi wenyewe wanasema "Kulipa kodi ni uzalendo"
Wasitufanye sisi kuwa ni mazuzu. WALIPE KODI ili wawe na uchungu na nchi yao
 
Mkuu unaweza ukawa na point kubwa sana, hapa hoja ni working class, haijalish ni private au public, hakuna kisingizio cha hovyo nilichowahi kusikia kama hiki cha kuwa ATM kutoka kwa mbunge mwenye privilege zote za diplomats
Ipo haja ya kuwabana zaidi, wengi sio kusinzia tu lakini hata hoja wanazojenga ni urojo wa kutisha, hivi kuna haja gani kuwa na watu wa aina hii ambao hata hawasomi wanachotakiwa kuchangia au kuzungumza? jamii ianze kuwakataa wabunge wa hovyo namna hii( kwao maslahi tu na wala si kwa wananchi waliowachagua)
Hii mijitu ni milafi safi. Magufuli kata kodi hao
 
Back
Top Bottom