Watumishi wa umma na kusoma/kujiendeleza

Status
Not open for further replies.

Mr. Teacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
330
Reaction score
88
KANUSHO: Serikali yakanusha kuhusu likizo isiyo na Malipo kwa Wanaoenda Kusoma

Kumekuwa na waraka unasambazwa mitandaoni uliotolewa ktk halmashauri moja huko Katavi ambao unaeleza kuwa mtumishi wa umma akitaka kujiendeleza kwa hatua ya shahada ya kwanza anapaswa 1. kujigharimia mwenyewe. 2. kuchukua likizo ya bila malipo kwa muda ataokuwa masomoni.

Watu wengi wameonyesha kushabikia hiyo taarifa, wachache wameonyesha kushangazwa na kutoelewa.

Mimi niwashangae tu na kuwasikitikia (kama kweli Serikali ina mpango huo) wale wote wanaoshabikia haki na stahiki za watumishi kuporwa. Lakini pia nisaidie kuwafafanulia ndugu zanguni; kwa mujibu standing order, mwajiri ana wajibu wa kumuendeleza mtumishi, kwa kuandaa mpango wa mafunzo, kutenga fungu la fedha ili kuweza kugharimia masomo ya mtumishi wake na kumlipa mtumishi mshahara wake kama kawaida. Hivyo wale mnaoshabikia bila kujua na kupotosha ukweli tafuteni standing order muisome muielewe. Lakini, kama Serikali hii ina lengo hilo na watumishi wakikaa kimya, na vyama vya wafanyakazi vikikaa kimya utakuwa mwanzo wa ukandamizaji mkubwa sana wa haki.
 
Mi sijaelewa kitu, je ni halmashauri zote au ni huko nsimbo pekeake (katavi) Sababu waraka unaosambazwa ni wa nsimbo, inawezekana ni maamuzi ya halmashauri yao tu au ni agizo kutoka ngazi za juu?
 
Kumekuwa na waraka unasambazwa mitandaoni uliotolewa ktk halmashauri moja huko Katavi ambao unaeleza kuwa mtumishi wa umma akitaka kujiendeleza kwa hatua ya shahada ya kwanza anapaswa 1. kujigharimia mwenyewe. 2. kuchukua likizo ya bila malipo kwa muda ataokuwa masomoni.
watu wengi wameonyesha kushabikia hiyo taarifa, wachache wameonyesha kushangazwa na kutoelewa.
Mimi niwashangae tu na kuwasikitikia (kama kweli Serikali ina mpango huo) wale wote wanaoshabikia haki na stahiki za watumishi kuporwa. Lakini pia nisaidie kuwafafanulia ndugu zanguni; kwa mujibu standing order, mwajiri ana wajibu wa kumuendeleza mtumishi, kwa kuandaa mpango wa mafunzo, kutenga fungu la fedha ili kuweza kugharimia masomo ya mtumishi wake na kumlipa mtumishi mshahara wake kama kawaida. Hivyo wale mnaoshabikia bila kujua na kupotosha ukweli tafuteni standing order muisome muielewe. Lakini, kama Serikali hii ina lengo hilo na watumishi wakikaa kimya, na vyama vya wafanyakazi vikikaa kimya utakuwa mwanzo wa ukandamizaji mkubwa sana wa haki.
Kwa trend ya mambo yanavyoenda siku hizi, akisimama Rais akatamka hivyo..hakuna mfanyakazi wala chama chake watanyanyua pua kubisha. Tumeshatengeneza nidhamu ya woga. Na tumeshakubali wenyewe kwamba Rais hawezi kukosea, what he says goes!
 
Mi sijaelewa kitu, je ni halmashauri zote au ni huko nsimbo pekeake (katavi) Sababu waraka unaosambazwa ni wa nsimbo, inawezekana ni maamuzi ya halmashauri yao tu au ni agizo kutoka ngazi za juu?
bado haijawa wazi, but may be, lisemwalo lipo!!!!
 
Kwa trend ya mambo yanavyoenda siku hizi, akisimama Rais akatamka hivyo..hakuna mfanyakazi wala chama chake watanyanyua pua kubisha. Tumeshatengeneza nidhamu ya woga. Na tumeshakubali wenyewe kwamba Rais hawezi kukosea, what he says goes!
Inabidi tusitengeneze mazingira ya namna hiyo; yeye ni binadamu pia, anaweza kukosea kama binadamu wengne pia. ktk hili naamini ni rumors tu, hawatotenda kinyume na standing order
 
Wasome online degrees kama uwezo unaruhusu, haina complications, self paced.. Yaan ni ww tu na speed yako

Utapiga pindi fresh na job unalisongesha kama umeme
sio kila degree inaweza kupatikana online; pia standing order iko clear tu, wala haizuii mtu kwenda shule na zaidi inaelekea jinsi mwajiri anavyowajibika kumsomesha mtumishi wake
 
Kwa trend ya mambo yanavyoenda siku hizi, akisimama Rais akatamka hivyo..hakuna mfanyakazi wala chama chake watanyanyua pua kubisha. Tumeshatengeneza nidhamu ya woga. Na tumeshakubali wenyewe kwamba Rais hawezi kukosea, what he says goes!
Ulichokiandika ni kweli. Kuna issues zilianza kama tetesi na baadae mkuu akaja kukandamizia. Usitishwaji wa ajira mpya ulianza hivi hivi, issue ya vijana wa udom nayo hivi hivi. Na akishalisema, Hata kama sheria za nchi zimekiukwa huwa tunabaki kama kondoo tu
 
sio kila degree inaweza kupatikana online; pia standing order iko clear tu, wala haizuii mtu kwenda shule na zaidi inaelekea jinsi mwajiri anavyowajibika kumsomesha mtumishi wake
Its true.. but kwa degree zinazopatikana online kama Business Administration/Management ni useful kwa mtumishi anayekosa muda wa kwenda evening classes.

Pia ni rahisi kupata ufadhili kwa online degree kuliko on campus cause ya online haina gharama kubwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom