Watumishi wa umma, atakayeshindwa kuwasilisha cheti kwa ajili ya uhakiki atakuwa amejiondoa kazini

marinji

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
417
484
Mtumishi wa Umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itakapofika tarehe 1 Machi, 2017atakua kajiondoa kazini mwenyewe.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah J. Kairuki alipokuwa akifungua mkutano wa watendaji Wakuu wa Wakala za serikali jijini Dar es saalm.

“Watendaji Wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki” amesema Kairuki.

Waziri Kairuki amewataka Watendaji Wakuu kuweka mikakati ya kuepuka watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwasababu jambo hilo limeumiza na kupoteza rasilimali fedha nyingi za Serikali.

Amesema anatambua kuna Wakala zenye upungufu wa Watumishi hivyo zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo ameelekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya mahitaji halisi ya Watumishi.

Aidha, pamoja na hilo ameelekeza Wakala zenye Watumishi wa mikataba zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya Taasisi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali. ikiwa ni pamoja na Watumishi hewa, taarifa chafu za Watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za Umma, kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro amezitaka Wakala za Serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania.


source. http://dar24.
 
Niliwaonesha uriginal certificates nikawaachia copies
Nikafanya hivyo kwa mara ya 2, 3 na ya 4.
Naamini sitakuwa miongoni mwao.
 
Hivi kuna nn na watumishi wa umma?

Hii sasa inaudhi na kuumiza mbona haya yameshafanyika?

Wana kila document ofisi za wakurugenzi wameitisha sana hizi nyaraka?
 
Kweli watumishi wa umma wameilewa na serikali wakishindwa waombe talaka
 
Hapo ina maana ajira hakuna mpaka baada ya uhakiki may duh....me nilijua february hii wanazimwaga
 
Inasikitisha sana mtu amefanya kazi kwa zaidi ya miaka thelathini amewafundisha kazi wengi tu waliomkuta kazini anakuja kufukuzwa bila malipo kwasababu eti aliongeza ka D kwenye cheti miaka 36 nyuma sioni usawa wa hili!! Wapo ambao walijituma na kujitoa sana kazini leo wanatoka patupu? kama mtu hakuwa na historia yoyote mbaya kazini tena alikua akisisifika kwa ufanyaji kazi bora maana experience ni moja ya vigezo kwenye ajira!! Wazungu wanasema If Experience Did Not Teach You Then School Won't Do!! Najua wapo wataosema natokwa povu itakua nami ni mtumishi wa umma hahahaha sifikirii kuajiriwa popote am boss of my own self mawazo yangu tu
 
Mtumishi wa Umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itakapofika tarehe 1 Machi, 2017atakua kajiondoa kazini mwenyewe. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah J. Kairuki alipokuwa akifungua mkutano wa watendaji Wakuu wa Wakala za serikali jijini Dar es saalm. [ 191 more words ]

http://dar24.
Nadhani sio watumishi wote. Huku kwetu kuna majina ya watumishi, yameletwa na waratibu kutoka tamisemi. Wanadai majina hayo yana utata hivyo yanapaswa kuhakikiwa tena.
 
Back
Top Bottom