Watumishi wa Serikali na siasa za mishahara

Mtoa mada nahis kuna kitu ulitaka kumaanidha kwa kundi flan la watumish wa serikali
Ila sio wote
 
Huduma gani isiyo leta tija hivi wewe mwalimu unayefundisha Area of Triangle au yule anayefundisha The quantity theory of money tangu mwaka 1995 mpaka leo ana saidia nini Taifa
Hiyo serikali inayo mlipa ndio iliyomwambia afundishe hayo wewe shida yako nini.Kujua nani ni mtumishi wa umma,na kazi za utumishi wa umma ni elimu ya chini sana ya uraia inatolewa mashuleni,kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.Mimi naamini mwanafunzi wa kidato cha pili aliyetulia shuleni na kuelewa civics ya kidato cha pili anakuzidi uelewa mbali na anaweza kukufundisha elimu ya uraia vizuri.Inawezekana una digrii wewe lakini bure.

Kuna watu wa aina yako humu huwa wanasema eti hakuna maana kuwa na watumishi wa umma,wakati huo tangu chekechea hadi chuo anahudumiwa na watumishi wa umma,anatibiwa na watumishi wa umma,wanaosimamia miradi yote mikubwa ya serikali,unayoiita ni maendeleo ni watumishi wa umma,wewe unaona umeme unawaka unadhani unatoka kwenye joto la tumbo lako?.Ninyi wenye elimu mnapoandika ujinga huu bila kujua unachokiandika,na bila kufanya utafiti wa unachokiandika ndio mnaodhalilisha elimu yetu ionekane ni duni,kama mtu hujui tu uraia wa kawida hivi,uliweza kweli ku-calculate hiyo pembe tatu?.Ni aina ya wanafunzi waliokuwa wanaweza kukariri nyimbo zote za bongo fleva, lakini wanashindwa kukariri maana ya biology ambayo haifiki hata mistari mitatu.

Labda wewe utusaidie wakati daktari na nesi wanamtibu mgonjwa ulitaka wawe wanazalisha nini hapo hosptalini, au kwa mgonjwa mwalimu wakati anakufundisha kusoma ulitaka awe anazalisha nini hapo shuleni au kutoka kwako.Ulitaka ustawi wa jamii wakati wanasuluhisha migogoro ya kifamilia wawe wanazalisha nini?.Serikali imeajiri watumishi wa umma ili wawahudumie wananchi,haija ajiri wafanyabiashara,wala wachimba madini.
 
Jamaa mleta mada vitumbua sana. Mfano nesi wa pale Muhimbili naye ni mtumishi wa umma, sasa azalishe zaidi vipi? Labda ukiandikiwa sindano moja, yeye akudunge tatu hapo atakuwa ame-ongeza uzalishaji wake.
 
Kutokuongeza mishahara kwa miaka hii yote mitatu haikuwa sawa!. Sasa wewe unakuja na hoja ya kupuunguza mimi ningekushauri ili tuokoe pesa za kutosha ya kujenga nchi washauri wenye mamlaka wawaondoe kabisa maofisini hawa wanaoitwa watumishi mfano waalimu, madaktari,manesi,polisi,wahandisi,wahasibu na wengine wote sisi watanzania tutafundisha watoto wetu kusoma tutatibu na kuuguza wagonjwa wetu tutakamata wahalifu wetu wazee wajadi watoa adhabu hapo unaonaje.
 
sasa kama ndo hivo tunaomba tufunge shule zetu zote,......
Huduma gani isiyo leta tija hivi wewe mwalimu unayefundisha Area of Triangle au yule anayefundisha The quantity theory of money tangu mwaka 1995 mpaka leo ana saidia nini Taifa
 
basi hata raisi na mawaziri wote tuwaondoe maana hawazalishi chochote.....aisee kuna ma zero brain nchi hii mpaka sio vizurii
 
aisee we Jamaa unajiona unauelewa mpana sana ila nikuambie ukweli wee ni bashite hadi nimeishiwa pozi
Hivi wafanyakazi mfano wa wizara ya kilimo hao wanaoitwa maafisa kilimo Dar Es Salaam Kinondoni kazi yao ni nini ? Wanaenda ofisi na kurudi halafu walipwe au

Afisa nyuki wa Ilala DsM anafanya nini kuna nyuki huko posta anaelekeza ?

Huna la kujitetea tofautisha wanaofanya Intangible services kama madaktari tunawapima kwa quality, Wengine mnapimwa kwa quantity
 
Huduma gani isiyo leta tija hivi wewe mwalimu unayefundisha Area of Triangle au yule anayefundisha The quantity theory of money tangu mwaka 1995 mpaka leo ana saidia nini Taifa
Sasa unategemea wakenya tutawapita kwa akili kama hii?? Piga picha hii mtu ndio imepewa mamlaka ya kufanymaamuzi ya kitengo fulani nyeti cha nchi. Watz tuombe sn
 
Povu unatoa là nini kwani nilikulazimisha kuwa mtumwa wa serikali

Muajiriwa yeyote wa serikali na mtumwa mnategemea kodi za walalahoi wakilipa na wasipolipa, Subirini 2018 biashara zikigoma ndio mtajua maisha ni nini ? Tunafunga biashara utalipwa na Babu yako
Biashara zik8goma kwani serikali inasimama kufanya kazi, hata kukopa itakopa 2
 
Back
Top Bottom