Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,160
Kipo kisa cha mfalme mmoja katika biblia aliitwa Rehoboamu,mfalme huyu alianza kutawala baada ya baba yake mfalme Suleiman kufariki.Mfalme Suleimani nyakati fulani katika ufalme wake alioa lundo la wanawake inakadiriwa kuwa 1000,na pia aliendekeza mambo ya anasa kwa kiwango cha juu,ili kufidia anasa zake aliwatoza kodi kubwa wananchi wake na kuwatumikisha sana na hivyo mpaka anafariki wananchi hawakuwa na furaha sana kama ilivyokuwa mwanzoni mwa ufalme wake.
Baada ya kifo chake ndipo mwanawe Rehoboamu alipochukua hatamu za uongozi,Wana wa Israeli wakiongozwa na Yeroboamu wakamfuata mfalme na kumuomba awapunguzie utumwa mgumu ambao baba yake alikuwa amewatumikisha,mfalme akawaahidi waje baada ya siku tatu ili apate ushauri toka sehemu mbalimbali kabla ya kuwajibu,wazee wakamshauri awe mwema,awapendeze na kuwaambia maneno mazuri,lakini vijana wakamshauri kinyume chake wakamshauri aendelee kukaza na kuwabana zaidi raia,mfalme akaupenda ushauri wa vijana,Baada ya siku tatu wana wa Israeli walipokuja kuchukua majibu, mfalme akawajibu kwa kiburi kwa kutumia ushauri wa vijana akasema:
'Baba yangu aliwafanyia kongwa zito nami nitawaongezea,baba yangu aliwapiga kwa mijeledi lakini mimi nitawapiga kwa nge'.Huo ndio ulikuwa mwanzo wa taifa la Israeli kupasuka vipande viwili -Israeli na Yuda.(unaweza soma kisa hiki katika kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati sura ya 10).
Yaliyotokea kati ya watumishi wa serikali waliokopa HESLB na serikali yao tulivu na sikivu yamenikumbusha kisa hiki,wakati watumishi hao wakiwa wanalilia ongezeko la mishahara na malipo ya madai yao mbalimbali kama likizo,gharama za kupandishwa vyeo na kubadilishwa/ kupandishwa madaraja na wakati watumishi hao wakililia ugumu wa maisha walichoambulia ni kuchapwa na NGE,makato yamepandishwa kwa asilimia saba zaidi kinyume hata na makubaliano yao ya awali,nahisi huu ni mwanzo tu wa 'kuishi kama mashetani'.