Watumishi housing comp ya nani?

Watumishi housing comp ya nani?

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,023
Reaction score
36,879
Kuna jengoo liko magomeni

Kwambele kuna tangazo watumishi housing comp NA kuna chats ya gov pembeni

Labda kwa mnaouja ni mbadala wa national housing ama.MDOGO MTU

Imeonyesha miradi kama ya nhc

Ahanteni
 
Nadhani ni taasisi ya selikali maana kuna mradi mwingine wa nyumba zaidi ya 50 nimeziona wamejenga kule bunju,,, mbele ya mradi wa TBA
 
Kama ni mbadala wa NHC basi wanajitahidi mana wanafyatua nyumba za kiwango cha lami tofauti na store za NHC..hawa WHC wako vizuri hata ramani zao zinavutia japo nadhani kuna watu wenye njuruku wana ubia hapa
 
Niliwahi kusikia ni mradi wa watumishi wa NHC...
 
Nijuavyo ni kampuni ya serikali yenye jukumu la kujenga nyumba zenye gharama nafuu na kuwauzia watumishi wa serikali. Imeanzishwa kama miaka mitatu hivi iliyopita huku wawekezaji katika kampuni hiyo wakiwa ni mifuko ya jamii kama PPF, PSPF, GEPF, NSSF na pia NHC.

Baadhi ya miradi yake ni kama huo wa Magomeni jirani na kituo cha Usalama, nyumba zilizojengwa kule Bunju/Mabwepande jirani na mradi wa nyumba za Tanzania Buildings Agency (TBA) na pia viwanja walivyopewa waathirika wa mafuriko ya miaka kama mitano iliyopita au viwanjwa vilivyokuwa vikiuzwa hivi karibuni na halmashauri ya manispaa ya Kinondoni.
 
Kampuni ya Nyumba za Watumishi (WHC) ni taasisi ya Umma ambayo ilianzishwa mwaka 2013. Kampuni hii inayojihusisha na uendelezaji miliki na usimamizi wa uwekezaji katika miliki.

WHC inatekeleza Mpango wa Taifa wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na ina jukumu la kujenga nyumba 50,000 zitakazouzwa kwa mikopo nafuu ya muda mrefu kwa watumishi waishio ndani na nje ya nchi. Mradi huu utakuwa katika awamu tano na utekelezaji wa ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2014/2015.

Kama msimamzi wa uwekezaji katika miliki, kampuni hii pia ina jukumu la kusimamia vipande vya uwekezaji katika miliki (REITs). Uwekezaji katika miliki ni aina mpya ya uwekezaji katika Tanzania na uwekezaji huu unatoa fursa lukuki kwa watanzania wote kushiriki na kuboresha kipato chao na kuleta maendeleo ya kiuchumi. WHC inakusudia kufanya kazi na wadau wa ndani na walioko nje ya nchi katika kukuza soko la uwekezaji katika miliki katika namna ambayo kila mtu atanufaika.

WAMILIKI WA WHC




Kwa taarifa zaidi tafadhali: Watumishi Housing Company
 
Back
Top Bottom