Bailly5
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 16,402
- 35,083
Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema wamebaini watumishi hewa 209 ambao wameisababishia Serikali hasara ya Sh 2.9 bilioni.
Awali, mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa 17.
Kutokana na ongezeko la watumishi hewa, Makonda aliwaapisha wakuu wa idara za mkoa na manispaa tatu na kuwapa wiki moja kuhakiki iwapo kuna wengine kwenye maeneo yao.
“Awali wakuu wa Idara hao walihakiki watumishi hewa 17 ambao waliingizia (Serikali) hasara ya Sh330 milioni. Baada ya kuwabana maofisa hao tumepata watumishi hewa 209 ambao walilipwa Sh2.9 bilioni, kutokana na hili nimetoa wiki moja wawe wamekamilisha kuhakiki,” alisema Makonda.
Chanzo: Mwananchi