Watumishi 15 wa Manispaa ya Bukoba watumbuliwa majipu

Watumishi 15 wa Manispaa ya Bukoba watumbuliwa majipu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,714
Watumishi 15 wa Idara za Ardhi, Mipango Miji na Ujenzi katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera akiwemo Msanifu wa Majengo wa Manispaa hiyo, Abukar Issa, wanashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma za kugawa hati ya ardhi kinyume cha Sheria ya Ardhi ya Mwaka 2004.

Agizo la kuwakamata watumishi hao limetolewa na Mkuu wa Mkoa, John Mongella kutokana na kikao cha dharura alichokiitisha ofisini kwake baina yake na watumishi hao wa idara hizo.

Mongella alisema amewaita ofisini kwake watumishi wote kutoka idara za Ardhi, Mipango Miji na Ujenzi kutaka kujua ni nani alitoa kibali kwa mmiliki wa kiwanja hicho kilichopewa namba 09 L kinachopatikana katika Barabara ya Uganda mjini Bukoba, huku watumishi hao wakionekana kutupiana mpira.

Alisema watumishi hao walikuwa wakitambua kuwa kiwanja husika kipo katika hifadhi ya Mto Kanoni ambao umekuwa ukiathiriwa na ujenzi holela na kuhatarisha uchafuzi wa mazingira katika Ziwa Victoria.

Kiwanja hicho ambacho kiliguswa na safishasafisha ya Desemba 9, mwaka huu siku ya maadhimisho ya Uhuru ambayo katika mkoa huo yaliambatana na usafi na uondoshaji wa makazi yaliyo ndani ya mita 60 kutoka katika hifadhi ya mto Kanoni unaopeleka maji yake ndani ya Ziwa Victoria.

Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Bukoba, Catres Rwegasira naye alikuwa na maswali ya kujibu mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa huo, Nassor Mnambila na Mkuu wa Mkoa huo.

Rwegasira alisema kwa mujibu wa sheria mpya ya ardhi ya mwaka 2004, hairuhusiwi mtu yeyote kuendesha shughuli wala kuweka jengo katika eneo hilo la mto ndani ya mita 60.

Naye Ofisa Msanifu wa Majengo, Abubakar Issa alipohojiwa na mkuu huyo wa mkoa kuhusu nani alitoa kibali cha ujenzi katika kiwanja hicho wakati wakijua kuwa ni makosa; Issa alikubali kuwa yeye ndiye alihusika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba, Aron Kagulumjuri alisema Manispaa hiyo ilikwishapiga marufuku ujenzi katika kiwanja hicho kinachopakana na mto huo, lakini hajui ni namna gani taratibu zilikiukwa.

Mkuu wa mkoa alisema watumishi hao 15 wamechukuliwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Bukoba kwa uchunguzi zaidi na endapo yeyote atabainika na shtaka kujibu hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa.
 
Lukuvi na Simbachawene naona hapa ndo pakuanzia hakikisheni hawa washenzi wanaondolewa katika utumishi wa umma.
 
Hakuna sheria ya ardhi ya mwaka 2004 mkuu. Sheria za ardhi zipo mbili, namba 4 na namba 5 zote za 1999.
 
Lukuvi na Simbachawene naona hapa ndo pakuanzia hakikisheni hawa washenzi wanaondolewa katika utumishi wa umma.

madai yathibitishwe kwanza kukurupuka sio public administration
 
sheria namba 4 1999 namba 5 1999 lakini zimefanyiwa marekebisho 2004!!!acha kukurupuka
 
madai yathibitishwe kwanza kukurupuka sio public administration

attachment.php


Alishabomolewa tokea wiki iliyoisha.
 

Attachments

  • Kanoni.JPG
    Kanoni.JPG
    26.5 KB · Views: 2,259
sheria namba 4 1999 namba 5 1999 lakini zimefanyiwa marekebisho 2004!!!acha kukurupuka

Wewe ndo unakurupuka. Inaitwa marekebisho ya sheria ya ardhi no.2 ya mwaka 2004. Hakuna sheria ya ardhi ya mwaka 2004.
 
mbona kuna ofisi ya ccm hapa Arusha iko mita kama tano hivi kutoka mtoni ni jirani na Hoteli ya Naura Spring, hapo napo vipi? nani alitoa hati?
 
Simbachawene anapo pa kuanzia.Akomae nao hawa Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa.Hawa ndio 'wanaoatamia' madudu kwenye maeneo yao!
 
Sasa unawapeleka polisi wakati wamekubali! Kwani sheria za utumishi si zipo au! Kwa sasa standing Order haifanyi kazi sasa kila kitu police.
 
ombi langu naomba wahusika wa hili swala, waliangalie kwa umakini kwani mungu hapendi kunyanyasa binadamu mwenzako.
 
Wewe ndo unakurupuka. Inaitwa marekebisho ya sheria ya ardhi no.2 ya mwaka 2004. Hakuna sheria ya ardhi ya mwaka 2004.

Nafikiri aliyeripoti alimaanisha sheria ya usimamizi wa mazingira ya 2004 ndiyo yenye kuzungumzia hizo mita 60...Sheria za ardhi zinabaki kuitwa na4 ya ardhi na 5 ya ardhi ya vijiji za 1999 pamoja na marekebisho yake.
 
Back
Top Bottom