Watumiaji nishati, maji kutafutiwa mwanasheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumiaji nishati, maji kutafutiwa mwanasheria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi.  Watumiaji wengi wa nishati na maji hawajui sheria, hali inayowafanya kushindwa kupata haki zao wanapopatwa na matatizo.
  Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma hizo (Ewura CCC), Profesa Jamidu Katima, alipofungua mkutano wa mabaraza ya mikoa ya Ewura CCC.
  Alisema Ewura imeweka utaratibu mzuri unaomwezesha mtumiaji kukata rufaa katika mamlaka mbalimbali za juu, ikiwamo Tume ya Ushindani anapoona hatendewi haki, lakini wengi wa watumiaji hao, huishia ngazi za chini. Profesa Katima alisema Baraza hilo lipo kwenye mchakato wa kutafuta mwanasheria, ambaye atakuwa anatoa ushauri kwa watumiaji, ambao hawakutendewa haki ili kuondokana na tatizo hilo. Alisema kuanzishwa kwa mabaraza ya mikoa, kutatatua baadhi ya changamoto zinazolikabili baraza, ikiwamo tatizo la elimu kwa watumiaji. Alisema jukumu hilo litafanywa na wawakilishi wa mikoa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema mkutano huo utawasaidia wawakilishi wa mikoa kubadilishana uzoefu wa kupata mbinu mpya.
  Naye mwakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB) nchini Kenya, Rosemary Rop, alisema wataendelea kushirikiana na Baraza la Ushauri kuhakikisha mtumiaji na mlaji anapata haki stahili.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...