Watumia mauji ya Mwangosi kutapeli

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000

amka2.gif

WATU wanaosadikiwa kuwa matapeli, wamekuwa wakimpigia simu mpiga picha mkuu wa gazeti hili, Joseph Senga, na kujitambulisha kuwa maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa wakitaka wakutane naye kwa madai ya kuchukua maelezo yake kuhusu tukio la mauji ya aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Senga ndiye alikuwa mpiga picha pekee aliyeshuhudia tukio hilo Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo na hivyo picha zake zimekuwa zikitumiwa na vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, taarifa za matapeli hao kutaka kukutana naye kwa mahojiano zaidi zilimshangaza kwa vile kesi hiyo iko mahakamani na hivyo kama ni ushahidi angeitwa kuutolea mahakamani.
“Mimi nilihojiwa na kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, nikaeleza kila kitu nilichokishuhudia siku ile, sasa nilishangaa kusikia watu hawa wakinipigia simu na kudai wanataka kuhojiana na mimi,” alisema.
Akisimulia mkasa mzima, Senga alisema kuwa watu hao wawili walianza kumpigia simu kwa nyakati tofauti wiki hii wakidai wanataka kukutana naye kwa mahojiano hayo.
“Mmoja alijitambulisha kuwa ni Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Iringa na kudai kuna ofisa mmoja amemtuma Dar es Salaam kwa ajili ya kuonana na mimi akiniambia kuwa amempa namba yangu,” alisema.
Senga alisema kuwa awali alianza kuwaamini kwani huko nyuma wakati Kamati ya Nchimbi ikiendelea na kazi, waliwahi kumpigia simu wakidai watakuja kuhojiana naye.
Hata hivyo, watu hao licha ya kuahidi kufika jana ofisini, hawakuja kufanya hivyo na hata baadaye walipopigiwa simu walikuwa wakijifanya wametingwa na kazi na hivyo wangelikuja wakati mwingine.
Tanzania Daima ilijaribu kuifuatilia moja ya simu zilizokuwa zikipigwa mara kwa mara ambayo ni 0715 695771 na kubaini imesajiliwa kwa jina la Musa Mahundi ambaye alikuwa akijitambulisha kama ofisa wa polisi kutoka Iringa.
Baada kuona ubabaishaji huo, ofisi ilimshauri Senga kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ili kujua kama kulikuwa na utaratibu kama huo lakini naye akaonekana kushangaa.
Kamuhanda alikana kumtuma mtu yeyote Dar es Salaam kufuatilia suala hilo na kusisitiza kuwa hana taarifa zozote za upelelezi huo huku akimtahadharisha Senga kuwa makini wa watu hao.
Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na bomu wakati akitimiza majukumu yake ya kuripoti ufunguzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kijiji cha Nyololo, ambapo askari polisi mmoja anashtakiwa kwa mauaji hayo.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom