Watuhumiwa JKT wasomewa mashtaka upya, warudishwa rumande

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wahitimu sita wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko usio halali na kushawishi wenzao kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa Umoja wa wahitimu hao, George Mgoba, Makamu Mwenyekiti, Parali Kiwango, Katibu Linus Steven na wahitimu wengine, Emmanuel Mwasyembe, Ridhiwani Ngowi na Jacob Mang’wita.

Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Respicius Mwijage, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Benard Kongola amesema, washitakiwa hao wanadaiwa kwamba Februari 15,2014 katika eneo la Msimbazi Centre, Ilala Dar es Salaam, walipanga njama za kutenda makosa hayo.

Katika shitaka lingine watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kuandamana kwenda kwa Rais kulazimisha kupewa ajira katika utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na lingesababisha uvunjifu wa amani.

Kwa upande wa mshitakiwa Mgoba, Kiwango na Steven, wanadaiwa siku hiyo katika eneo hilo, walishawishi wahitimu wenzao wa mafunzo ya JKT, kufanya maandamano kwenda kwa Rais kulazimisha wapewe ajira katika utumishi wa umma jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani ikiwa ni siku chache baada ya kesi dhidi yao kufutwa na kuachiwa Mei 26, mwaka huu kisha kukamatwa tena na leo kupandishwa mahakamani kwa mashtaka hayohayo.

Katika kesi ya awali iliyokuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, tayari mashahidi saba walikuwa wameshatoa ushahidi mahakamani hapo huku akiwa amebakia shahidi mmoja tu ili kufunga ushahidi ndipo kesi hiyo ilipofutwa na watuhumiwa hao kukamatwa tena na kusomewa mashtaka hayo.

Watuhumiwa hao wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Juni 9, mwaka huu.

JKT-watuhumiwa.jpg
 
Dola ni dola tu.. ukijitia ujasiri kwa ushabiki wa magazeti mwisho wa siku likibuma huwaoni..unanyea mtondoo peke yako
 
Wamekatwa, wamefikishwa mahakamani na pengine kuadhibiwa kwa kosa LA kudai kupata kazi ambayo ni haki yao.

Kama hiyo haitoshi wanasiasa wanawaahidi vijana ajira ila wanaopewa wala hawaombi au kuandamana kama ilivyotokea mkoani arusba mwanzoni mwa mwaka huu.

Badala ya kutumia nguvu kubwa kuwashitaki kwanini hamkuwapeleka sums jkt yenye malindo lukuki hapa nchini?
 
Kuchuchumalishwa ni sawa na kuwadhalilisha hawa vijana, they aren't proved guilty mpaka sasa.

Huyu George pamoja nakufanyiwa unyama lakini bado anahenyeshwa vilivyo, hii case inabidi iishe haraka maana inaweza trigger hasira kwa JKT wengine maana ni wengi sana kitaa.

Kupambana na government ni sawa na kumnywesha mmbwa uji utapata taabu yet hujui adui yako halisi ni nani.

Soldier hagomi sijui hawa vijana hawakuelewa hii topic kipindi cha mafunzo.
 
Ndugu zangu mnaoenda JKT kwa kujitolea,JKT haiajiri,ikitokea umemaliza miaka yako miwili bila ajira ukubaliane na hali ilivyo
 
Wamekatwa, wamefikishwa mahakamani na pengine kuadhibiwa kwa kosa LA kudai kupata kazi ambayo ni haki yao.

Kama hiyo haitoshi wanasiasa wanawaahidi vijana ajira ila wanaopewa wala hawaombi au kuandamana kama ilivyotokea mkoani arusba mwanzoni mwa mwaka huu.

Badala ya kutumia nguvu kubwa kuwashitaki kwanini hamkuwapeleka sums jkt yenye malindo lukuki hapa nchini?

kazi haidaiwi kwa kuandamana!.. unasubiri tangazo litoke unaomba kama wanavoomba wengine!...

ingalikuwa kila mwanachuo anapomaliza tu, anaandamana kulazimisha ajira sijui tungefika wapi
 
Wamekatwa, wamefikishwa mahakamani na pengine kuadhibiwa kwa kosa LA kudai kupata kazi ambayo ni haki yao.

Kama hiyo haitoshi wanasiasa wanawaahidi vijana ajira ila wanaopewa wala hawaombi au kuandamana kama ilivyotokea mkoani arusba mwanzoni mwa mwaka huu.

Badala ya kutumia nguvu kubwa kuwashitaki kwanini hamkuwapeleka sums jkt yenye malindo lukuki hapa nchini?
Usiongee kitu usicho kijua.
Jkt form ya mkataba inasema wazi kuwa Jkt haiajiri, mtu huwe tayari kurudi nyumbani mkataba wako utakapo isha.

Hakuna sehem walipoahidi ajira.
Kuajiriwa ni matokeo tu
 
Back
Top Bottom