Watu Zaidi ya 200 Kutoa Ushahidi Kesi ya Ubunge

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mashahidi 239 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao katika kesi Namba 6 ya 2015 ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoani Songwe Japheti Hasunga(CCM)

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Fanuel Mkisi

Mashahidi hao wataanza kutoa ushahidi wao March, 7 mwaka huu, ambapo upande wa mlalamikaji watakuwa 74, mshitakiwa 85 na Jamhuri watakuwa 80.

Wakili wa mlalamikaji Boniface Mwabukusi alieleza mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya kuwa alisema katika shauri hilo atawaleta mashahidi 74 kwa ajili ya kutetea hoja za maombi ya mteja wake.

Naye wakili anayemwakilisha mlalamikiwa ambaye ni Mbunge wa jimbo la Vwawa Japhet Hasunga, Sambwee Shitambala alipoulizwa idadi ya mashahidi atakaowafikisha mahakamani hapo kutetea shauri hilo alisema anao mashahidi 85 na akaiomba Mahakama wasitajwe majina yao mahakamani, badala yake watakuwa wakitajwa mara tu wanapohitajika.

Kwa upande wake wakili mkuu wa serikali, Joseph Pande aliiambia mahakama kuwa upande wa Jamhuri utakuwa na mashahidi 80 ambao watafika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

Akiahirisha shauri hilo Jaji Dyansobera ameziasa pande zote kuwa mahakama imezingatia kuwa kesi za uchaguzi zimewekewa muda maalumu wa kuzisikiliza chini ya kifungu cha 115 cha sheria ya uchaguzi kuwa kesi hizo zinapaswa kumalizika ndani ya miezi 12 na pia kwa mujibu wa maelekezo ya Jaji Mkuu zinapaswa kuwa zimemalizika ifikapo Juni mwaka huu, hivyo kesi hiyo itapaswa kusikilizwa mfululizo.

Ili kuendana na muda uliopangwa, Jaji huyo amezitaka pande zote tatu kuhakikisha zinapeleka mashahidi kwa wakati mara tu watakapohitajika ili kuipa nafasi mahakama kutimiza wajibu wake kwa muda uliopangwa na hapo akaahirisha shauri hilo Marchi 7 mwaka huu litakapo tajwa tena.
 
Haki itendeke haiwezekani uanze kupokea mshara wa kodi za wananchi wakati hawakukubali.
 
Mbona kesi za ubunge za CCM dhidi ya CHADEMA na CUF haziletwi wala kujadiliwa humu JF?
 
ya kafulila imeshaaje kwanza .. kama sio kutuchezea hapa .. or mara watu 80.. hata wakiwa 1090000 hizo kesi ni upotevu tu wa hela kama hawez shinda mtu hapo
 
kuna tetesi kwamba shitambala hajawahi kushinda kesi yoyote aliyoisimamia katika kipindi cha miaka 10 , kama ni kweli hii ni fedheha sana .
 
Back
Top Bottom