Watu Wema na Waovu

Ubuntu trusty tahr

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
326
Reaction score
228
Habari wakuu nimekuwa nikisikia dhana ya mtu mwema kuwa ni yule anayetenda matendo mazuri yanayompendeza Mungu kila uchao vivyo hivyo dhana ya mtu mwovu ni kuwa yeye daima anatenda matendo mabaya yanayomchukiza Mungu mpaka atakapoamua kubadilika na kumrudia Mungu"" ninachokiona kwenye ulimwengu wa sasa hao waoitwa watu wema huwa mambo yao yanakwenda taratibu sana hata mafanikio yao huwa yanachelewa sana kwani kila wakati wao wanaingiwa na hofu ya kupita njia za panya ili kufikia mafanikio na malengo kwa kipindi kifupi wao muda mwingi wanaamini katika kutenda mema tuu:::::hao wanaoitwa watu waovu mafanikio yao huwa ni ya haraka sana kwani hawaoni tabu kufanya vitendo vinavyoitwa viovu ili kufikia mafanikio kwa uharaka . tafakari kuhusu mafanikio ya watu wanaopiga madili ,watu wanaotoa kafara, watu wanaodhulumu wengine watu watu wanaofanya ubadhirifu watu wanaofanya vitendo vya hujuma nk watu hao huwa wanapata mafanikio kwa haraka sana "

Kwa tafsiri nyingine ukiwa mtenda mema usitegemee sana kupata mafanikio hapa ulimwenguni zaidi sana tegemea hasara toka kwa ndugu jamaa na marafiki "" @nimtazamo tuu cc wakuu wote wenye mioyo migumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maaana Wahenga wakasema, TAJIRI KUUONA UFALME WA MBINGU NI SAWA NA NGAMIA KUPITA TUNDU LA SINDANO. Siri za Utajiri ni vichaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…