Watu wasiojulikana wachoma nyumba tano, ofisi ya CCM na kituo cha Afya Pemba

Void ab initio

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
5,720
5,659
Watu wasiojulikana wamechoma moto Kituo cha Afya, nyumba 5 za wananchi na ofisi ya CCM Kisiwani Pemba usiku wa manane.

Chanzo; ITV
 
Kuna Amani kwanza kunawanajeshi wengi tumeimarisha ulinzi atakayeleta fyoko fyoko atutacheza nae wamesahau akuna nchi ambayo jeshi lishawai kushinda nguvu ya wananchi
 
Watu wasiojulikana wamechoma moto Kituo cha Afya,nyumba tano za wakaazi na Afisi ya CCM huko Kibirizi,Pemba.

Habari zaidi zitafuata kadiri zitakavyopatikana

Chanzo:Radio One breaking news
 
Kumekucha na karatasi zao feki za kupiga kura picha ya maalim sefu yatumika
 
Kuna Amani kwanza kunawanajeshi wengi tumeimarisha ulinzi atakayeleta fyoko fyoko atutacheza nae wamesahau akuna nchi ambayo jeshi lishawai kushinda nguvu ya wananchi
Hao wanajeshi walikuqa wapi wakati hao watu wasio julikana wanachoma moto nyumba za wananchi, kituo cha afya na ofisi ya ccm? kuwepo kwa wanajeshi na walinda amani zanzibar hakumaanishi kama fujo hazitotokea kwa sababu hapo watakuwa wanaviziana tu askari akienda kulia muharifu anaenda kushoto kwa kweli zanzibar inahitaji maombezi na duaa la sivyo tutasikia mengi ya kutisha huko.
 
Wazanzibari wanajuana kwa vilemba, Jeshi halitaleta suluhu kama wanavyodhani, wanasahau kuwa unaweza lazimisha punda kwenda mtoni lakini akifika huko huwezi kumlazimisha kunywa maji
 
Maafa hayo yametokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa kumi usiku ambapo kamati ya ulinzi na usalama kisiwani humo imethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo: ITV habari za saa.
 
Mpaka ifike tarehe 20 zitaungua sehemu nyingi sana, tuendelee kusubiri matukio ya syria, na nchi hii ilvyo pembezoni mwa bahari na juzi NVY wamekiri wana vifaa hafifu, tutaona mengi.
 
Back
Top Bottom