Watu wanne wameuawa katika maandamano nchini Cameroon

Watu wanne wameuawa katika maandamano nchini Cameroon

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Takriban watu wanne wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya upinzani yaliyofanyika Jumapili Oktoba 26, 2025 mjini Douala, Cameroon, ambapo Waandamanaji walikuwa wakilalamikia madai ya wizi wa kura kufuatia uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12.

Mgombea wa upinzani Issa Tchiroma, ambaye alichuana na Rais Paul Biya katika uchaguzi huo, ndiye aliyeitisha maandamano hayo, huku tume ya uchaguzi nchini humo ikitangaza kuwa matokeo kamili ya uchaguzi yatatolewa leo Jumatatu Oktoba 27, 2025

Soma Viongozi wawili wa Upinzani Wakamatwa Cameroon, Tchiroma atoa wito Maandamano ya Kitaifa

Tchiroma amedai kupata asilimia 54.8 ya kura, ingawa wachambuzi wengi wanatarajia Rais Biya, mwenye umri wa miaka 92, kushinda muhula wa nane. Wakosoaji wa serikali hiyo wanasema mfumo wa uchaguzi nchini humo umejaa dosari na hauakisi demokrasia ya kweli.

Tchiroma, ambaye ni Waziri wa zamani na aliyewahi kuwa mshirika wa karibu wa Rais Biya, alijitenga na kiongozi huyo na kuamua kuwania Urais kama mgombea huru. Uamuzi ulioibua mvutano mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Kwa mujibu wa gavana wa mkoa wa Douala, waandamanaji walishambulia vikosi vya jeshi na vituo vya polisi katika wilaya mbili, hali iliyosababisha vifo vya raia hao wanne na majeraha kwa maafisa wa usalama, hali iliyo ongeza wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini humo

Maandamano kama hayo yameripotiwa pia katika miji mingine Nchini humo ikiwemo Yaounde, Maroua na Bafoussam, ikiwa ni ishara ya kuenea kwa hasira miongoni mwa wananchi wanaotilia shaka uhalali wa uchaguzi. Taarifa zinasema Serikali ya Taifa hilo haijatoa tamko rasmi kuhusu vifo hivyo hadi sasa

1761545890356.png

=============

Four killed in Cameroon protests ahead of election results, opposition says

DOUALA, Oct 26 (Reuters) - At least four people were killed by gunshots in opposition protests in Cameroon's commercial capital Douala on Sunday, according to the campaign of presidential candidate Issa Tchiroma, who is seeking to oust veteran leader Paul Biya.
Tchiroma called for the protests to demand that the results of an October 12 vote be respected, a day before the outcome is due to be announced.



Source: Reuters & BBC
 
Kwetu ni keshokutwa tukatiki kwa amani turudi nyumbani kusubiri matokeo. Tuweke rekodi nzuri asife au kuumizwa hata mtu mmoja. Tutunze amani ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom