Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
KUSEMA NA KUFANYA
Wote tunajua kusema sana kuliko kufanya.
Kuna watu wanasema na wanafanya, ila changamoto inaanzia hapa, wanachosema wanafanya sio kile wanachokwenda kufanya.
Wanasema hiki na wanafanya kingine.
Kwa kuanzia fikiri kila mtu anakwenda kufanya tofauti na kile anachosema atafanya, halafu angalia ni jinsi gani unaweza kushawishi afanye kile ambacho kweli amesema atafanya.
Bila ya wewe kuweka ushawishi ni vigumu sana kwa mtu mwenyewe kufanya kile alichosema atafanya.
Na elewa hapo nimesema ushawishi na sio nguvu, maana utakapoweka nguvu utamfanya atake kufanya hovyo zaidi.
Kuamini tu mtu anaposema na wewe ukaenda na yako, unatoa nafasi ya kuangushwa au kuumizwa.
Hali hii ipo kwenye kila eneo la maisha ambapo mtu mwingine anakuahidi wewe kufanyia kitu halafu hafanyi.
Usitoe ahadi kama huwezi kuitimiza.