Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma(PPRA) imemruhusu ,mkuu wa kitengo cha sheria cha PPRA, Bertha Soka kuendelea na utumishi wa umma licha ya yeye kujumuishwa katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mtumishi huyo,mkurugenzi wa zamani wa ATCL,David Mataka na Mrurugenzi wa zamani wa PPRA,Dr Ramadhan Mlinga.
Mkurugenzi wa sasa wa PPRA,Dr. Laurent Shirima alipoulizwa alisema huo ni uamuzi wa Bodi ya PPRA ambayo ndio mwajiri wake na kwamba yeye hawezi kuupinga na ameongeza kuwa Bodi ilipitia sheria na kanuni za utumishi wa umma na kuona kuwa hata kama Soka anatuhumiwa bado anaweza kuendelea na kazi zake na kwamba hakuna sababu za kumsimamisha
Chanzo:Nipashe online