Watu wakimya/wapole njoeni tuambiane shida/changamoto zilizotukuta au zinazotukuta

Binafsi ni mpiga Makelele. Mtukutu, Mchokozi, mkorofi Yaani sipendi sehemu itulie hata siku moja.

Kipindi Tunasoma Boarding tulikuwa tunatabia ya kuamka usiku wa manane. Tunaenda kuchukua ngoma za UKWATA. Tunarudi Bwenini tunapiga ngoma tunacheza tukiwa na Viboxer tuu.

Hapa watu wataamka na kutukemea lakini tumo. Au tugonge kengele usiku wa manane yaani kwa kweli mimi napenda Life la kashi kashi. Sipendi utulivu hata siku moja.

Hata hapa kitaa huwezi simama na demu wa kitaani kwetu alafu wewe ni mtu wa kuja.

Napenda tabia yangu kwa maana tunaifanya jamii ichangamke. Tunawapa kazi polisi.

Pia tunaamini ndio tabia halisi ya kiume. Sio unazubaa Zubaa kama Zombi
Nimekupenda bure

We sio fata mkumbo
 
kwenye kudai ni kazi kwa kweli,,kuna siku nilishindwa kumkopesha pesa mtu nikwambie sina(namkopeshaga ila akipata humuoni)
roho iliniuma aisee ,baadaye nikamuuliza ulipata, nikampa nusu....

kama umekopesha halafu ni mpole kwenye kudai fanya kama umetoa sadaka tu.........
Nikopeshe laki 5 mkuu
 
Nadhani wengi huwaona wana ringa hasa kutokana na jamii kuwa na uelewa mdogo. ila kwenye mahusiano ni watu wanapata mteremko sana kwa watoto wa kike. Yaani wanawake huwasumbua haswa kwani mara nyingi huwa wapo serious kwenye relationship(committed) and they rarely cheat. Changamoto za mahusiano, Wanawake hutegemea makubwa sana kutoka kwao.

All in all from my observation ni watu wenye changamoto ku link na jamii hasa na vijana na watu wenye umri wa kati ila huaminika sana ndani ya jamii kwani Wazee na watu wenye busara huwaamini kwa kuwa morally huwa wapo vizuri ukilinganisha na wengi.
 
Binafsi nje ya JF ni mkimya yani kama hujaniuliza kitu mimi huwezi kuniona najibu mixer aibu kupindukia na muonekano wa kipole japo sio mpole kabisaaaa

Changamoto kubwa ni kuonekana naringa wakati sio kweli
Daah mimi mpole changamoto ni kila mtu ananipenda sina adui ...
 
Kwenye kuoa nayo inakuwaje? Kama wewe ni mkimya inabidi uuoe angalau muongeaji la sivyo humo ndani patakuwa hapakaliki. Wangu ameshafaham tabia yangu, mimi napenda kumsikiliza zaidi na nikimjibu maneno siyo mengi.
 
Kwenye kuoa nayo inakuwaje? Kama wewe ni mkimya inabidi uuoe angalau muongeaji la sivyo humo ndani patakuwa hapakaliki. Wangu ameshafaham tabia yangu, mimi napenda kumsikiliza zaidi na nikimjibu maneno siyo mengi.
Yeah ni vizuri ikiwa hivyo ila muhimu zaidi kwenye mahusiano ni mtu kupata mtu anayekuelewa. Ukipata mtu anayekuelewa jua umepata embe Dodo sio wengi ambao wenye bahati hiyo, Hii ina apply kwa jinsia zote.
 
Sisi wakimya inatusaidia kusoma mchezo kabla ya kukurupuka,pia upole ni silaha ya kutoingiwa kirahisi ovyo ovyo maana inakuwa kama defensive mechanism hadi mtu akuzoee
 
Siye wengine hadi kuambiwa tunajisikia tumeshazoea, japo mwanzo hilo neno lilinikwaza sana nikaanza kujitahidi kucopy na watu ila nilishindwa nikaamua kubaki tu nilivyo. Watu wameshasema weeh! mpk wamechoka.
Lakin wanaonijua vizuri wanajua mie siyo mpole hvyo kabisa, shida ni sizoeleki kirahisi..
 
Mkuu hiyo changamoto nimeipitia hasa kwa wawanawake unapofanya vurugu zako hadi anashangaa Kama ni wewe unayemjua au vipi. Lakini pia ni la usiri, Mimi nilidate na mtoto wa kike tangu nipo form two na nikiwa form nikazaa naye mtoto, watu wamekuja kujua ukweli nikiwa University, lakini Bibi yangu hadi kesho anakataa kuwa siyo kweli nasingiziwa kuhusu huyo mtoto( nimelelewa na Bibi tangu mdogo sana hadi Leo). Na hadi Leo ukiacha mchizi wangu mmoja wa kitaa hakuna mtu aliwahi kuniona nikiwa na huyo dada, lakini nilikuwa nabutua karibia kila wikiend hasa kuanzia form 2 hadi 4.
Na wapole na wa kimya mara nyingi hupati shida kutongoza, yani unaweza kung'oa demu mkali ukala mwaka mzima ndio watu wakagundua, sababu huwa hatuna showoff.

Yani mtu mpole kama unataka demu we kuwa na namba yake tu! Mkichat kidogo utasikia anakwambia nataka siku nije kukutembelea, hapo kimebaki nini tena? Akija unajifanya kama kumasogelea unashangaa anaonesha ushirikiano. Akifika kwao anakwambia hivi nani kakufundiha huu utundu.
 
Hahahaaaa wew hatari

Yaani hii tabia imenishinda kuacha, uzuri JF imenibadilisha sana, kabla ya kuingia kwenye argument nahakikisha nimefanya references zote ili nisichemke.

Na nikichemka nakubali kushindwa, yanaisha. Smartphone pia kwenye google imenipunguzia ubishi.
 
Back
Top Bottom