Moja ya maarifa ya siri ya zamani za kale ilikuwa ni sehemu moja katika uwili ina maarifa juu ya sehemu ingine lakini haiwezi kufanya moja kwa moja.
Hivyo watu wa zamani wakajifunza Maarifa ya kuungana na sehemu ya siri ili kupata elimu juu ya mambo mengi na iwe fahari na msaada katika maisha ya sehemu yao.
Kilicho kuwepo ni kwamba watu walijua kuwasiliana na mambo ya sirini yaani viumbe wa huko ili kupata uelewa zaidi.
Taaluma ya mawasiliano na viumbe wa upande wa pili ilikuwa taaluma ya siri zaidi kuliko zingine zozote kutokana na mtu akiweza zoezi hilo alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya na kuwa kwa namna nyingi kufuata maelekezo ya kiumbe wa sirini.
Watu wakajifunza taratibu na mambo mengi ya kujenga na ya kubomoa, wengine wakafanya siri na urithi kwa vizazi vyao.