Watu wa zamani #7

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
Katika uwili watu wa zamani walitambua kua kama kuna vitu vinavyo onekana basi vipo vitu visivyo onekana, wakasema ikiwa kwenye mwanga ni sehemu ya vitu kuonekana basi ni sehemu ya maisha kwa vitu kuonekana na kwenye giza ni sehemu ambayo hata kama kuna vilivyopo havionekani kabisa kwa macho ya nyama kutokana na giza na maisha hayo yanabakia kuwa siri kwa bayana ya macho ya nyama.

Watu wa zamani wakaendelea kuthibitisha uwili katika mimea. Wakaona sehemu ya matawi huonekana dhahili lakini sehemu ya mizizi ipo ardhini pasipo onekana na uhusiano wa namna hiyo ukafanya uhai wa mmea kila sehemu ikiwa na majukumu yake.

Wakaona hata mbegu ili iote na kustawi kwa usahihi inafunikwa na udongo gizani huko inaanza na mizizi kisha sehemu ya pili matawi.

Watu wa zamani wakaenda mbali wakaona mtoto hadi kuzaliwa na mama yake anaanza kutengenezwa gizani kwenye tumbo la uzazi la mama kwa muda na wakati maalumu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…