Maendeleo ni utaratibu au matokeo mapya zaidi ya jambo lililokuwepo.
Kitu kinaweza kuwa hitaji lako kwa ajili ya kufanikisha utulivu flani, kika kufanikishia utulivu huo kila wakati na ukajua ndio hivyo hivyo jinsi ilivyo kumbe kuna zaidi ya hivyo usiyo ijua wewe.
Mtu anaweza kuishi karibu na mawe ambayo ni madini ya thamani kwa jambo flani na asijue kama mawe ya karibu yake hayo ni thamani kwa jambo flani, yeye akachukua na kuweka kama mapambo katika mazingira yake akijua na kufahamu kwamba ndio kinacho yastahili mawe hayo.
Mtu huyo mwenye kuishi karibu na mawe akaja kutembelewa na mtu ambaye ni wa kiroho katika makazi yake hayo na amwambie habari ya mawe yaliyo karibu naye kuwa mawe haya ni mamlaka za kiroho, zilipo mamlaka hizi roho wa machafuko , malazi na mambo flani hawawezi kabisa kusogea, na mamlaka hiyo ndio inayofanya familia iwe na afya njema, mifugo izaliane na mambo mengine.
Lakini pia aje mtu wa mambo ya teknolojia hapo kwenye makazi ya mtu mwenye kuishi karibu na mawe na amwambie mawe haya ni hodari sana kwenye mawasiliano kwa namna hii na hii.
Basi mtu huyo mwenye kuishi karibu na mawe hayo kuanzia hapo baada ya maarifa kuhusu mawe anayo ishi karibu nayo, atachukulia mawe hayo tofauti na siku zingine zilizo pita na atakuwa ameendelea katika maarifa juu ya hayo mawe.