ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Niliona video yake youtube alivyoenda znz Ali enjoy. Nafikiri watu wa airport walitakiwa wajue sheria kwenye hayo masuala ya viza
Siku hizi kidogo wamejitahidi zamani airport kuombwa nje nje
Huyu mwanamke ni juhaa tu. Kuna vitu lazima hakuwa navyo. Watz sio watu wabata kiasi hicho. Je kuna rushwa? Yes ipo. But kama alikuwa na docs sahihi hawawezi kumzuia.
Terminal 3 kiongozi pale kunawaka cheche stage ya kufuka moshi imepita tayari.Na kuibiwa wanaibiwa!!! Ile Airport ni ushenzi
kuombwa rushwa kwani labda tu ilikuwa inshu ya kutoelewana ila sidhani kama ni rushwa.
Unaongea hivyo ikiwa hata Burundi tu hujafika suala kama hilo ni janga kwa Africa nzimaHuyu mwanamke ni juhaa tu. Kuna vitu lazima hakuwa navyo. Watz sio watu wabata kiasi hicho. Je kuna rushwa? Yes ipo. But kama alikuwa na docs sahihi hawawezi kumzuia.
Hivi wewe Mkuu kuna wakati unaipa akili yako likizo, maana kuna wakati unatoa point sana, then unakuja boa sana. Vipi kulikoni? Mie nidanganye inisaidie nini?Sio kweli uongo
Sio kweli uongo
Mkuu uko sahihi kabisa , hawa jamaa wengi wao ni mbumbumbu wa kutupwa. Kuna mambo nimekutana nayo Uhamiaji yanasikitisha hata kusimulia.
Nadhani wengi mnakumbuka kisa cha yule Mkenya ambaye aliingia nchini kupitia Namanga, na akiwa Tanzania akataka kusafiri kwenda Europe kwa kupitia airport Dar JKNIA kwa ajili ya safari ya kikazi. Uhamiaji pale airport walimwambia haiwezekani kwa sababu aliingia kwa gari kupitia Namanga hivyo inabidi atoke nchini kwa kupitia Namanga tena.
Watu wa airline walibishana sana na uhamiaji, wakijaribu kuwaelimisha ikashindikana, na ikabidi jamaa ashushwe toka kwenye ndege. Aliporudi Kenya alisambanza email kuhusu umbumbumbu wa Migration officials Tanzania.
Mie binafsi mara nyingi nimesafiri kupitia Nairobi kwenda Europe, nikipitia Namanga kwa kibasi kwa kuwa nakuwa Arusha ambapo ni karibu na Nairobi kuliko kusafiri hadi Dar. Sijawahi kupata matatizo kwenda Europe kupitia Kenyatta airport kwa kuwa niliingia Kenya kupitia Namanga! Nilishangaa Migration wetu walimwambia jamaa lazima arudi kwanza Namanga alikoingilia!