Watu wa Airport watoe majibu, Tanzania Migration inawekwa doa Youtube na tourist wa African American

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,941
3,860
Kwakweli nimepita Youtube and I came across video moja. Ni mdada wa Kimarekani akilalamikia migration ya airport terminal 3 kuwa ni corrupt, na walitaka kuchukua rushwa, kwani maofisa hao walimzuia kusafiri kutoka Tanzania kwenda Nigeria kwa sababu zisizojulikana.

Watu wa nchi mbalimbali katika comment section wameisema sana vibaya nchi yetu, wengine ni majirani kabisa, haya mambo tusiruhusu yakatokea yanatuchafulia wakati ndo tunaanza. Tunataka huyo afisa aliye mhudumia huyu dada pamoja na uongozi wa Airport waje watoe majibu.

Mpaka inafikia watu wa nje wanamshauri akareport kwa Magufuli kwa kuwa wanajua Raisi wetu si mtu wa kulea rushwa.

Nina mashaka pia na tuhuma za huyu dada wa kimarekani za kuombwa rushwa kwani labda tu ilikuwa inshu ya kutoelewana ila sidhani kama ni rushwa.

Embu wote tukajionee tulivosemwa vibaya , pia tulivochambwa kwenye comments,

 
Niliona video yake youtube alivyoenda znz Ali enjoy. Nafikiri watu wa airport walitakiwa wajue sheria kwenye hayo masuala ya viza
Siku hizi kidogo wamejitahidi zamani airport kuombwa nje nje

Dah tumechafuka hatari, na huyo dada alijaribu kuuliza nani mkuu hapa aweze kumsaidia, nasikia akasema yeye ndo senior, so wengine wote walikuwa wanashangaa tu. Sasa ile video inazunguka dunia nzima
 
Huyu mwanamke ni juhaa tu. Kuna vitu lazima hakuwa navyo. Watz sio watu wabata kiasi hicho. Je kuna rushwa? Yes ipo. But kama alikuwa na docs sahihi hawawezi kumzuia.

Umesikia aliyoeleza haswa mwanzoni alivyokuwa navyo? Cha kujiuliza ni kwanini wanamzuia akiwa ana yote aliyoambiwa awe nayo na hizo nchi zingine na docs alikuwa nazo?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Airport wanaajiri tu bila kuangalia mengi, hii ni aibu. Lazima kuna wengine haya yamewakumba.

Baada ya kuomba pesa (eti fee kwa cash no receipt) na kumfata hadi kwenye ATM na akaomba details zake za credit card, duh!!! Staff wa aiport wamekuwa na njama hizi siku hizi za wizi, WOW!!!
 
  • Masikitiko
Reactions: rr3
Kuna siku Watu wa Uhamiaji pale airport walimzuia abiria kurudi kwao eti kwa sababu aliingia Tanzania kupitia Namanga kwa hiyo lazima atoke kurudi nchi yake kupitia Namanga! I say nilibaki hoi. Alijaribu kujieleza alipitia Namanga baada ya kutembelea Kenya, kisha akaenda Ngorongoro na kuja Dar es Salaam hadi Zanzibar sasa alikuwa anarudi nyumbani. Wapi bwana, walimgomea. Ndio nikajua Tanzania kuna watu vihiyo sio kawaida - akili ndogo mamlaka makubwa kama baba yao!
 
Kuna mambo ya ajabu sana pale,siku niko kwenye foleni na madogo fulani Yule Jamaa migration kwanza kawaita kimkwara Nyie njoeni hapa wanaenda kinyonge ,then kamwita bwege mwingine na mishati yao litumbo hilo kaja kawachukua Wale madogo kaenda nao chooni huko nafkiri walimalizana maana madogo walitoka kivyao jamaa nae katoka kivyake,Ndio Naona Wale mayanki Wanakuja panga foleni ku check inn,

Very strange,ila nikakauka tu inawezekana wanajuana Lakini tu ile kuona waliniharibia mood kabisa maana kuna siku km hao madogo nilipigwa euro 250 hapo airport Na afisa mmoja anaitwa mujalwisi Sijui Na wenzie wawili.
Yaani rushwa ya kulazimisha maana walinikalisha toka sa saba mpk sa 1 jioni.
kosa hamna km hao wamehamishiwa uwanja mpya ndo hayo tunayaona.
 
Huyu mwanamke ni juhaa tu. Kuna vitu lazima hakuwa navyo. Watz sio watu wabata kiasi hicho. Je kuna rushwa? Yes ipo. But kama alikuwa na docs sahihi hawawezi kumzuia.
Unaongea hivyo ikiwa hata Burundi tu hujafika suala kama hilo ni janga kwa Africa nzima
 
Ni mambo ya ajabu sana, mambo kama haya yanachafua taswira ya nchi hayakemewi wala hakuna anaejali.

Kukosa professiinalism kunaligharimu sana taifa hili. Tunasafari ndefu.
 
Sio kweli uongo


Mkuu uko sahihi kabisa , hawa jamaa wengi wao ni mbumbumbu wa kutupwa. Kuna mambo nimekutana nayo Uhamiaji yanasikitisha hata kusimulia.

Nadhani wengi mnakumbuka kisa cha yule Mkenya ambaye aliingia nchini kupitia Namanga, na akiwa Tanzania akataka kusafiri kwenda Europe kwa kupitia airport Dar JKNIA kwa ajili ya safari ya kikazi. Uhamiaji pale airport walimwambia haiwezekani kwa sababu aliingia kwa gari kupitia Namanga hivyo inabidi atoke nchini kwa kupitia Namanga tena.

Watu wa airline walibishana sana na uhamiaji, wakijaribu kuwaelimisha ikashindikana, na ikabidi jamaa ashushwe toka kwenye ndege. Aliporudi Kenya alisambanza email kuhusu umbumbumbu wa Migration officials Tanzania.

Mie binafsi mara nyingi nimesafiri kupitia Nairobi kwenda Europe, nikipitia Namanga kwa kibasi kwa kuwa nakuwa Arusha ambapo ni karibu na Nairobi kuliko kusafiri hadi Dar. Sijawahi kupata matatizo kwenda Europe kupitia Kenyatta airport kwa kuwa niliingia Kenya kupitia Namanga! Nilishangaa Migration wetu walimwambia jamaa lazima arudi kwanza Namanga alikoingilia!
 
Eat Love Migrate ndio YouTube Chanel yake, Nazani video zake zote alizokuwa Tanzania niiziangalia,alienjoy sana Zanzibar,Dar kariakoo,alienda Arusha nazani karatu aliishi Takribani wiki,baadae Kilimanjaro akakutana na Mdada mwingine(Travelling Sista) akawa mwenyeji wake akamtembeza sana alikaa napo siku nyingi.kwa kifupi Mimi nilifatialia video zake maana napenda sana Ndugu zetu wanao hamasisha wausi warudi afrika, alivyozuiwa Airport niliumia sana sana,Nauli Yake ilikufa na hakuna wakum-refund.Kuna maboya wako Airport wanachafua image ya hii nchi,natamani huyo mtu ningemjua apewe hata fundisho maana kama ni nchi yetu huyu Dada kaitangaza sana,watu wengi wamehamasika kuja Tanzania kwa ajiri yake kwa jinsi alivyokuwa anapasifia,maana alienda kuishi hadi kijiji flani huko Arusha.
 
Kama raia wa Marekani anataka kutoka Tanzania aende Sierra Leone, halafu mnasema hana ndege ya kutoka Nigeria kwenda Sierra Leone, kwa nini hilo liwe issue kwa uhamiaji ya Tanzania kumuacha Mmarekani huyu aende Nigeria?

Kwa nini azuiwe kutoka Tanzania? Kama anaenda Nigeria halafu atapanda basi kutoka Nigeria kwenda Sierra Leone tunajuaje?

Akifika Nigeria, ataka younganisha safari kwenda Sierra Leone sisi inatuhusu nini?

Akiamua kubaki Nigeria na kuolewa hapo, sisi inatuhusu nini?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom