Watu sita wamekamatwa na silaha mbili za kienyeji na risasi 23 mkoani Mwanza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na silaha mbili zilizotengenezwa kienyeji pamoja na risasi 23, ambazo walikuwa wakizitumia katika matukio ya unyang’anyi wa mali na uporaji katika jiji la Mwanza na mikoa mingine.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu kamishina Ahmed Msangi amesema silaha hizo zimekamatwa katika eneo la Buswelu wilayani Ilemela zikiwa zimefichwa kwa mganga wa kienyeji aitwaye Leonard Litta anayeishi mtaa wa Kagida, kufuatia msako mkali uliofanywa nyumbani kwa mganga huyo na askari sambamba na kukamata risasi 22 zinazotumiwa na bunduki aina ya Short Gun pamoja na risasi moja ya Rifle aina ya Mark IV.

Katika tukio jingine, kamanda Msangi amesema watu wawili Rahim Feka mkazi wa Ilala na Ally Kawalale mkazi wa Jetrumo Airport Dar es Salaam wamekamatwa katika eneo la Ilemela wakiwa katika harakati za kuuza gari lenye namba T.778 AZV aina ya Toyota Land Cruiser wanalodaiwa kuliiba huko Ilala jijini Dar es Salaam.

Aidha kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina Ahmed Msangi amesema msichana aitwaye Dema Charles mkazi wa Kandawe wilayani Magu ameuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kiunoni na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala, huku wenzake wawili wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Halikadhalika, jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa Kigoma Ahmed Gambo, mwenye umri wa miaka 22 baada ya kukutwa akiwa amevaa sare za jeshi hilo katika eneo la Igogo Bugarika jijini Mwanza, ambazo zinasemekana aliziiba kutoka kwa askari H.6362 PC Mriha wa Ofisi ya RPC Mwanza, wakati askari huyo akiwa msikitini kwa ajili ya kufanya ibada.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom