SoC03 Watu, Siasa na Maendeleo

Stories of Change - 2023 Competition
Jun 3, 2022
13
13
WATU, SIASA NA MAENDELEO
Watu ni Wananchi, Wananchi ni watu wanaotambulika kisheria kitaifa katika serikali au jimbo la kawaida iwe kuomba au kuzaliwa. Kwa uelewa Wangu mdogo najua kuwa Raia na Mwananchi/Wananchi wote ni kitu kimoja. Kigezo kikuu cha sehemu iitwe nchi basi ni lazima kuwe na Raia yaan watu. Watu ndio wanaweza kufanya shughuli zote katika nchi kama vile Shughuli za kisasa, shughuli za kijamii na Jinginezo. Hivyo nchi ili iwe na maendeleo inahitaji Raia wengi Tena wenye Elimu na utashi kwa maendeleo ya nchi.

SIASA
Siasa ni shughuli ya kimaadili inayohusiana na ujengaji wa jamii Yenye usawa. Hii ni maana aliyoitoa mwanafalsafa mkubwa Duniani Aristotle, Pia akadai kwamba binadamu ni mnyama wa kisiasa anayeishi kwenye jamii ya kisiasa hivyo kila kitu ni siasa. Vijana wengi wa Kitanzania nmesikia wakisema ohh mimi sipendi Siasa kwa sababu Siasa ni mchezo mchafu halafu huyo huyo akikaa kijiwen anaanza kulalamika ety ohh Ajira Hakuna na maisha yanazidikuwa magumu. Kamwe wewe kijana mwenzangu usijesema ety mimi sipendi Siasa halafu badae ulalamike na ugumu wa maisha, katika ulimwengu huu Hakuna nchi itapata maendeleo bila yakuwa na vijana wanaopenda na kuwajibika juu ya Siasa ya nchi yao. Kama unapenda uwe na Ajira na uwe na maisha mazuri basi ni lazima ukubali kuwajibika katika Siasa ya nchi yako maana kila kitu ni siasa kama alivyosema Aristotle.
Zifuatazo ni faida za Vijana kuwajibika juu ya Siasa ya nchi yako.

i. Kuwa Mzalendo. Mara kadhaa tumesikia kuwa uzalendo katika nchi yetu ya Tanzania umepungua Hilo nakubaliana nalo kabisa na linatokana Sana na vijana pamoja na Raia wengi kutokuwajibika katika Siasa za nchi ndio maana sikuhizi Utasikia vijana wakisema "BONGO BAHATI MBAYA" au wengine wakisema "BORA KUZALIWA MBWA ULAYA" hii yote inatokana na kutokuwajibika katika Siasa za nchi.

ii. Kuthamini Utamaduni wetu. Mara nyingi tumesikia Wazee wakisema kuwa vijana wa sikuhizi hawana maaadili kabisa. Ni kweli lakini chanzo cha hayo yote ni Kutokuwajibika katika masuala yote ya Siasa maana kila kitu katika jamii zetu ni siasa hivyo hata kuporomoka kwa maadili inatokana na suala la kuchukulia Siasa kama ni kitu cha kawaida.

iii. Kujali Rasilimali za nchi. Vijana wengi siku hizi imekuwa kawaida Sana kuiba vifaaa vya ujenzi pindi mradi Fulani wa kiserikali unapojengwa kwa faida ya Wananchi wote. Rasilimali hizi ni faida ya nchi nzima lakini vijana wamekuwa hawathamini kabisa mpaka kuiba vitu hivi na hii hutokana na kutokuwa Mzalendo na nchi yako na chanzo kikuu kutokuwajibika katika Siasa za nchi yetu.

iv. Kuongozwa kwa Haki, kama Wananchi wote tutakuwa msitari wa mbele katika kufatilia Siasa ya nchi yetu hivyo ni lazima tutaongozwa kwa Haki na usawa na sikwa ubabe na Ukiona nchi fulani inaongozwa kibabe basi ujue Raia wa nchi hiyo hawawajibiki ipasavyo katika kufatilia Siasa ya nchi yao.
Na madhara yakutofatilia Siasa ya nchi ni kama ifuatavyo

i. Ufisadi, Kama hatutakuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha Siasa ya nchi yetu inaenda mbele basi ni lazima tutaibiwa tu na Hawa viongozi wetu ndio maana Mara kadhaa tumesikia Kuhusu skendo ya ESCROW, EPA na Ufisadi mwingine mwingi huu unachangia na sisi watanazania wenyewe kutokuwa na ufuatiliaji wa Siasa yetu.

ii. Kutokuwajibika kwa Viongozi wetu,Nchi ya Tanzania ni moja ya nchi ambayo viongozi wetu hawawajibiki ipasavyo katika kutekeleza yale tuliyowatuma na hii inatokana na uchache wa Raia kufatilia Siasa ya nchi yetu na hio hufanya viongozi wawe wavivu Sana

iii. Kuwepo kwa Upendeleo katika Ugawaji wa mahitaji ya kijamii, ni dhahili kwamba baadhi ya maeneo au mikoa Tanzania inahuduma nyingi Sana za kijamii na baadhi ya mikoa inahuduma chache Sana za kijamii kama vile shule hospital masoko na kadharika hii imekuwa ikitokana na viongozi kupendelea kwao bila kujali usawa wa masilimali hizi katika nchi nzima.

iv. Ubinafsishaji wa Mali za Uma, Mara nyingi Sana tumekuwa tukishuhudia viongozi wetu wakijimilikisaha Mali za Uma hasa migodi, mahospital na vitu vingine vingi, na hii ni kutokana na uzembe wa sisi Watanazania kutokuwa msitari wa mbele katika kujua nchi yetu inaelekea wapi na inataka nini.
Vijana wenzangu naomba Tusimame msitari wa mbele katika kupigania nchi yetu hasa katika Siasa ya nchi yetu kwa maana Siasa ndio chanzo cha maendeleo katika nchi yetu. Tuhimizane na Tushauriane juu ya umuhimu wa kufatilia Siasa ya nchi ili tuepuke kusema maisha magumu Mara ohhh Ajira Hakuna. Mimi kama Davis Abely Nziku aka DNA nitasimama msitari wa mbele katika kuhakikisha nafatilia Siasa ya nchi yangu kinaga ubaga yaani nje ndani Natumaini na wewe msomaji utakuwa kama mimi katika kufatilia Siasa ya nchi yetu Tanzania .

MAENDELEO
Maendeleo ni Hali ya kuwa na Mabadiliko Chanya, kutoka hatua moja ya kawaida na kwenda hatua nyingine bora na kubwa zaidi. Katika nchi ili iweze kuwa na maendeleo basi ni lazima iwe na watu Wasomi wenye Elimu zao na wenye utashi sahihi, watu tu hawatoshi ili uwe na nchi Yenye mafanikio basi unahitaji kuwa na Siasa bora Tena Siasa ya kisasa na sio ya mkoloni. Katika nchi yetu naona bado Kuna vitu vidogovidogo ambavyo vinaashiria uwepo wa Siasa ya kikoloni ndio maana hatufanikiwi kama nchi nyingine ambavyo zimefanikiwa. Nnaposema SIASA YA KIKOLONI namaanisha Hivi

i. Uchu Wa Madaraka. Katika nchi yetu tuna majimbo ambayo toka Enzi za mwalimu mpaka Leo inambunge huyo huyo mmoja hata haijawahi kutokea akaacha kugombea na ukiangalia jimbo lake halina maendeleo kabisa. Huu wote ni siasa ya ukoloni ya kutaka uwe wewe tu Kwan Hakuna wengine?

ii. UBABE na Uhaba wa DEMOKRASIA . Katika nchi yetu hatuna kitu kinachoitwa Demokrasia licha ya nchi yetu kuwa ni ya kidemokrasia lakini mimi sikubaliani kabisa sababu Mara nyingi tumeona kura zikiibiwa katika chaguzi na kupelekea kutokuwepo kwa usawa kabisa baina ya nchi na vyama vya kisiasa.

iii. Viongozi Kujiona Mungu Mtu. Viongozi wengi Sana wa kitanzania wanajiona kama wao ndio kila kitu katika nchi hadi inapelekea kutudharau sisi Raia wao ambao tumewapa vibali vya kutuongoza.

Hivyo Basi kama tunataka nchi yetu Tanzania iwe na maendeleo inahitaji Hawa viongozi wetu waache Siasa ya kikoloni Mara moja na tuingie kwenye Siasa ya kisasa ili tupate maendeleo kama nchi nyingine za ulaya.
Siasa watu na Maendeleo ni vitu ambavyo vinaenda sambamba katika kila hatua na katika kila amuzi Hivyo pendekezo langu kwa vijana wa Kitanzania tuwe na mwamko wa kufatilia Siasa ya nchi yetu na Viongozi wetu waache Siasa ya kikoloni ili tuweze kupata maendeleo kama ulaya. Nikiomba na kushukuru kwa Jina la Jamhuri...............................

Mimi ni Davis Abely Nziku (DNA)
Contact ;0755386540
0628488781
Mkazi wa Kigamboni Mjimwema
 
Back
Top Bottom