Watu na hali ya uchumi

Watu na hali ya uchumi

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,745
Reaction score
8,230
Nimejifunza duniani kuna aina mbili ya watu kwenye hali za uchumi; kuna wale wanaouliza bei ya bidhaa au huduma kabla hawajanunua na wale ambao wanachukua bidhaa au kutumia huduma wakiwa na na uhakika kuwa kwa gharama yoyote ile wanaweza kugharamia.....mimi ni mmoja ya wanaulizia bei ya bidhaa au huduma kabla ya kununua au kulipia tena nitabargain bei mpaka muuzaji akasirike...

Wewe upo kwenye kundi lipi?
 
Mimi kitu nikikipenda nakua nimesha amua kukinunua hata kabla ya kuuliza bei yake,pesa ni matokeo tu,tumia pesa ili utafute zingine.
 
Mimi huwa nanunua halafu nikifika Home najiuliza "hivi hii Bei niliyonunua nisahihi kweli au nimepigwa!"?
 
Unamaanisha bidhaa gani mkuu?
 
Hahahah umenikumbusha kuna siku nilienda kununua Kiatu mi na Rafiki yangu... tumefika eneo la tukio na nimenunua yeye akiwepo kila hatua hadi nikanunua wakati tunaondoka ananiambia MWANANGU HICHO KIATU UMEPIGWA dah!! kumlaumu nimeshindwa basi nikabaki kucheka tu
 
Ah ha haa haaaaa
 
Back
Top Bottom