Watu kumpenda Mungu katika shida tu

Watu kumpenda Mungu katika shida tu

Pastor Silla

Senior Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
162
Reaction score
166
Ukifanya utafiti watu wengi umkumbuka Mungu wakiwa wamekumbwa na shida na tabu mbalimbali. Mara nyingi hawana muda kumtafuta wakiwa kwenye raha au furaha. Jambo hili mara zote uwa linanipa uzuni sana kwamba kwanini Mungu amempa "utashi " mwanadamu maana huo utashi mwanadamu anaweza utumia kinyume na yeye au kuumbatana nae.

Tuangalie Warumi 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu ufanya kazi pamoja na wale mpendao katika kuwapatia mema,yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Andiko Hilo linatupa msingi kwamba ili Mungu aachilie mema yote kwetu anataka tukaze kumpenda yeye ambao hao ndio walioitwa kwa kusudi lake.Hali hii katika nykati zote wanadamu wengi hawampendi Mungu ila wanapenda vitu vyake hii ndio mara zote inapelekea Mungu kushindwa kuachilia baraka ambazo tunadeserve kuzipata kutoka kwake.

Niliangalia uzi wa ndugu Mshana Jr juu ya laana nimeona watu wengi waki-comment kwamba wana hizo changamoto katika familia wamejaribu kwenda makanisa ya kinabii au kilokole kuombewa lakini hakuna matikeo .Kwa uelewa wangu juu ya hao wandungu ni kwasababu hawamuendei Mungu kwa kusudi la kuitaji mahusiano nae thabiti kwa sababu yeye ni Mungu.Lakini wengi wanataka shida zao zitatuliwe ikiwa kutoka kwenye vifungo au umasikini n.k.

Ndio maana nyakati za Sasa Shetani amejua jinsi wanadamu walivyo amepandikiza manabii na Mitume wa uongo wanaohubiri baraka kuanzia Januari mpka Desemba na kuwauzia watu maji,mafuta,sabuni na leso za upako na watu hao hali zao kuzidi kuwa mbaya.

WATU wa nyakati za Sasa wanatakiwa wafahamu kwamba Mungu anatakiwa apendwe kwa viwango vikubwa na wafate amri zake kwa kushika na kutenda neno lake.Yohana 14:15 inasema vyema ukinipenda utazishika amri zake.Kwa hiyo basi ili Mungu aachilie baraka kwako yakupasa kumpenda na kuliishia neno lakekwa vitendo na usimwendee Kama yeye ni mganga wa jadi.

Mpe Yesu maisha na ukoke ndio mema yatakujia kubwa kuliko lote uupate uzima wa milele.

Barikiwa.
 
Ni hulka ya kiasili mno tunapokuwa njema kumsahau Mungu
 
Kwa hiyo Mungu anataka umpende kwanza ndio akubariki, usipompenda hakuna baraka, sio?

Maana yake baraka za mungu ni something for something, hakuna cha bure, ndio maana yake, sio?

Kwamba hapa Duniani kuna watu wameitwa kwa jina lake mungu, wengine hawakuitwa, hao ambao hawakuitwa ni kwa sababu gani?

Ni kwa nini mungu asubiri hadi watu wapate shida ndio wamkimbilie, kwa nini asizuie hizo shida kwanza, ama hawezi au hajui shida zinawatembelea satu wake wakati gani?
 
Wewe Mungu anatakiwa akutoze bili ya hewa yake unayoivuta, kila mvuto mmoja uwe ni senti 0.000001 tu.

Hapo ndipo utakapojua kwamba Mungu ni habari nyingine.
 
Kwa hiyo Mungu anataka umpende kwanza ndio akubariki, usipompenda hakuna baraka, sio?

Maana yake baraka za mungu ni something for something, hakuna cha bure, ndio maana yake, sio?

Kwamba hapa Duniani kuna watu wameitwa kwa jina lake mungu, wengine hawakuitwa, hao ambao hawakuitwa ni kwa sababu gani?

Ni kwa nini mungu asubiri hadi watu wapate shida ndio wamkimbilie, kwa nini asizuie hizo shida kwanza, ama hawezi au hajui shida zinawatembelea satu wake wakati gani?

Brother kitu ambacho hujawahi kukila kabisa ukisimuliwa na aliyewahi kukila ladha yake ilivyo utamuelewa kweli?
 
Kwa hiyo Mungu anataka umpende kwanza ndio akubariki, usipompenda hakuna baraka, sio?

Maana yake baraka za mungu ni something for something, hakuna cha bure, ndio maana yake, sio?

Kwamba hapa Duniani kuna watu wameitwa kwa jina lake mungu, wengine hawakuitwa, hao ambao hawakuitwa ni kwa sababu gani?

Ni kwa nini mungu asubiri hadi watu wapate shida ndio wamkimbilie, kwa nini asizuie hizo shida kwanza, ama hawezi au hajui shida zinawatembelea satu wake wakati gani?
Hakuna haki pasipo wajibu mpendwa ili upate haki lazima uwajibike like wise Mungu anachotaka kwetu ni easy only umpende Basi.

Pia zipo baraka za jumla kwa wale wanaompenda na wasiompenda uzipata mfano mvua,jua ,punzi n.k lakini zipo baraka za Ziada kwa wale wampendao katika kuhachilia mema yote na si kidogo ambazo wale wasimpenda uzikosa.

Kuhusu Mungu kuzuia shida amesha fanya hivyo kwa kutulipia deni la dhambi zetu msalabani ndio maana kwenye Mathayo 11:28 anasema "Njooni kwangu ninui nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo yeye atawapunzisha" .Wayu hawataki kupata raha kwa Yesu ndio maana bado wapo vifungoni.

Pia Mungu amesema anakwenda kutuandalia makao alipo yeye na sisi tuwepo (Yohana 14:1-8).Au tunaweza sema Mungu atuahidi kuwepo kwenye mbingu mpya na nchi mpya ambayo haina laana au shida na mikosi mbalimbali.Hiyo mbingu na nchi ijayo itajaa raha,amani na furaha maisha yatakuwa ya raha Sana.
 
Hata hivyo huwa hatuachi.Mungu ni mwema wakati wote.
Mungu anachelewA kuhukumu ulimwengu anataka watu wote wakimbilie toba .Kamata fursa toka kwa Shetani tupo mwishoni ndugu.
 
Kwa hiyo Mungu anataka umpende kwanza ndio akubariki, usipompenda hakuna baraka, sio?

Maana yake baraka za mungu ni something for something, hakuna cha bure, ndio maana yake, sio?

Kwamba hapa Duniani kuna watu wameitwa kwa jina lake mungu, wengine hawakuitwa, hao ambao hawakuitwa ni kwa sababu gani?

Ni kwa nini mungu asubiri hadi watu wapate shida ndio wamkimbilie, kwa nini asizuie hizo shida kwanza, ama hawezi au hajui shida zinawatembelea satu wake wakati gani?
Ukisoma Mwanzo 4 Mungu alimwambia Kaini je ukitenda vyema hutapata kibari.Means kwa Mungu fanya vyema utabaeikiwa pia angalia Kumb 28 zipo Baraka na laana pale ,Baraka kwa wale watakao fanya vizuri na laana watakao tenda vibaya.
 
Kwa hiyo Mungu anataka umpende kwanza ndio akubariki, usipompenda hakuna baraka, sio?

Maana yake baraka za mungu ni something for something, hakuna cha bure, ndio maana yake, sio?

Kwamba hapa Duniani kuna watu wameitwa kwa jina lake mungu, wengine hawakuitwa, hao ambao hawakuitwa ni kwa sababu gani?

Ni kwa nini mungu asubiri hadi watu wapate shida ndio wamkimbilie, kwa nini asizuie hizo shida kwanza, ama hawezi au hajui shida zinawatembelea satu wake wakati gani?
Before Mungu aliumba kila kitu chema na akampa utashi mwanadamu lakini mwanadamu aliposhindwa kumtii Mungu na kukengeuka dhambi ikaingia duniani na dhambi ikapelekea uovu na matatizo kujaa juj ya uso was Dunia.But Mungu ameahidi mbinguni mpya na nchi mpya isiyo na.mawaa ikiwemo magonjwa na shida zote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom