Watu hawa wanapata wapi hayo mamlaka ya "maagizo"?

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,710
Reaction score
4,046
Umekua ni utaratibu wa kawaida kabisa hapa nchini kwa watu wasiokua na mamlaka yoyote yale ya kiserikali kuagiza au kutoa oda kwa serikali kufanya jambo flani kwa mtazamo wao waonavyo, mfano; "Humphrey Polepole amekua akiiagiza serikali iwakamate watu flani au ichunguze jambo flani au anapenda kusema tu ninaiagiza serikali ifanye jambo flani".

Neno kuagiza ni oda, kinacho fuata ni utekelezaji tu ktk utaratibu,,, na ni watu wengi tu ambao sio chochote kimamlaka kwenye serikali hii na hawa wamekua wakiona nchi ni chama, kwamba na maagizo yao ni kama wanamwambia mwanachama wao tu.

Kwenye utawala wa nchi hatuangalii vyama vya siasa, ila tunaangalia sheria, na sheria hizi ndio zinazotoa nafasi na kuwapa watu mamlaka ya kutoa maagizo.

Polepole, Bashiru au wengine wowote ni third parties tu ktk mahusiano ya serikali na wananchi.

Jambo hili linakua sanaa, na matokeo yake wananchi wanaweza kuzidi kuwaogopa viongozi wa chama kama polepole kwa kuhofia kwamba polepole na wenzake wanaweza kuagiza wakamatwe kwa kadri watakavyo jiskia kwa kua wamezoea kuwaona kwenye vyombo vya habari wakitoa maagizo watu flani wakamatwe.

Samahani kwa mfano wa polepole, ila yeye ni miongoni mwa watu ambao wamekua wakinukuliwa sanaa kutoa maagizo/oda ya watu flani wakamatwe au wachunguzwe wakati hawana nafasi yoyote ile kwenye serikali ya nchi hii.

Kiutaratibu walitakiwe watumie neno "kuomba" nnaiomba serikali imchunguze flani! Na sio et nnaiagiza serikali kumkamata flani!.
 
CCM ndiye chama dola so kinayo haki ya kuiamrisha serikali,ni tofauti na vyama vingine wao "huomba"
 
Ni maagizo kutoka juu. Ahsante.
 
ila ni ktk awamu hii tu, awamu makini viongozi wake wa serikali hawawezi kuruhusu haya.
 
Umekua ni utaratibu wa kawaida kabisa hapa nchini kwa watu wasiokua na mamlaka yoyote yale ya kiserikali kuagiza au kutoa oda kwa serikali kufanya jambo flani kwa mtazamo wao waonavyo, mfano; "Humphrey Polepole amekua akiiagiza serikali iwakamate watu flani au ichunguze jambo flani au anapenda kusema tu ninaiagiza serikali ifanye jambo flani".

Neno kuagiza ni oda, kinacho fuata ni utekelezaji tu ktk utaratibu,,, na ni watu wengi tu ambao sio chochote kimamlaka kwenye serikali hii na hawa wamekua wakiona nchi ni chama, kwamba na maagizo yao ni kama wanamwambia mwanachama wao tu.

Kwenye utawala wa nchi hatuangalii vyama vya siasa, ila tunaangalia sheria, na sheria hizi ndio zinazotoa nafasi na kuwapa watu mamlaka ya kutoa maagizo.

Polepole, Bashiru au wengine wowote ni third parties tu ktk mahusiano ya serikali na wananchi.

Jambo hili linakua sanaa, na matokeo yake wananchi wanaweza kuzidi kuwaogopa viongozi wa chama kama polepole kwa kuhofia kwamba polepole na wenzake wanaweza kuagiza wakamatwe kwa kadri watakavyo jiskia kwa kua wamezoea kuwaona kwenye vyombo vya habari wakitoa maagizo watu flani wakamatwe.

Samahani kwa mfano wa polepole, ila yeye ni miongoni mwa watu ambao wamekua wakinukuliwa sanaa kutoa maagizo/oda ya watu flani wakamatwe au wachunguzwe wakati hawana nafasi yoyote ile kwenye serikali ya nchi hii.

Kiutaratibu walitakiwe watumie neno "kuomba" nnaiomba serikali imchunguze flani! Na sio et nnaiagiza serikali kumkamata flani!.
Serikali inatekeleza ilan ya Chama chake, kwaiyo wenye chama wanaweza kuielekeza/ kuikumbusha nin walitakiwa kufanya mwisho wasiku chama ndicho kinakutana na wananchi wakawida kwakua kina mizizi mbaka ngazi ya shina.
 
Back
Top Bottom