GE2025 Watu 9 washtakiwa kwa Uhaini Makambako, idadi yafikia watuhumiwa 196 nchi nzima

GE2025 Watu 9 washtakiwa kwa Uhaini Makambako, idadi yafikia watuhumiwa 196 nchi nzima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
Watu tisa wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe wakikabiliwa tuhuma za kosa la uhaini na kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 makosa ambayo waliyalifanya kwa kipindi cha kati ya mwezi March mpaka Octoba 30 mwaka 2025.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa serikali Magdalena Whella amesema watuhumiwa tisa akiwemo Erasto Nzenge (31) , Japhet Kimbe (27), Saimon Mlelwa (23) , Masondole Manyama (33), Stanley Mbembati (39), Anord Tunduru (30), Fadhil Nguvila (25), Patrick Mpagike (37) na Prosper Mbwilo (26) wanatuhumiwa kwa kosa la uhaini ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 384 cha mwenendo wa makosa ya jinai marejeo ya kifungu cha 16 cha mwaka 2023.

Washitakiwa hao tisa wamepandishwa leo Novemba 7,mwaka 2025 kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe na kusomewa mashitaka mawili ya kesi namba 26483/2025 mbele ya hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Njombe Mheshimiwa Matrida Kayombo.

Akisoma mashitaka hayo Mwanasheria wa serikali Magdalena Whella amesema kosa la kwanza ni kuwa kwa nyakati tofauti ya mwezi Machi mpaka tarehe 30 Oktoba mwaka 2025 katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Njombe walikula njama na kutenda kosa la Uhaini chini ya kifungu cha sheria namba 384 cha mwenendo wa makosa ya jinai marejeo ya kifungu cha 16 cha mwaka 2023.

Katika kosa la pili wakili wa serikali amesema washitakiwa hao walitenda kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39 cha pili cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 marejeo ya mwaka 2023, ambapo maelezo ya kosa ni kuwa washitakiwa mnamo tarehe 30 ya mwezi wa kumi mwaka 2025 katika mji wa Makambako walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kujiingiza kufanya fujo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za serikali zinazotumika kutolea huduma muhimu.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mawili, hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Matrida Kayombo amewataka washitakiwa hao kutojibu chochote hadi hapo shauri hilo likapokwenda kusikilizwa kwenye mahakama kuu,

Aidha upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika kwa makosa hayo mawili na kwamba makosa yote hayana dhamana na washitakiwa wamerudishwa mahabusu hadi tarehe 12 Mwezi wa Kumi na Moja mwaka 2025 kesi itakapo tajwa tena.

Pia soma GE2025 - Watu wengine 25 waongezwa kwenye mashtaka ya Uhaini Dodoma, idadi yafikia 187 nchi nzima

 
Kwa sheria zetu unaweza ukakohoa tu, ukapewa kesi ya uhaini

1762530258560.png
 
Uhaini imekuwa kosa la kawaida watu kutenda na watu wa kawaida.
 
Hakuna jipya, hata uchaguzi wa 2020 Magufuli aliagiza wote waliomtaa ccm kutangazwa washindi kwa shuruti wafungwe jela. Yaani mahakama inageuzwa chombo ya kunyamazisha wananchi dhidi ya chaguzi za kihayawani.

Hukumu tayari wanayo mahakimu, hapo walipo wanafanya maigizo ili wapime upepo kisha wawafunge bila hata ushahidi. Tuhakikishe 9 December tunatoka kwa wingi kwenye maandamano ili tumalize huu ushenzi.
 
Back
Top Bottom