Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa Tisa kwa tuhuma za kujiingizia fedha kwa njia zisizo halali kupitia mitandao ya kijamii pamoja na simu za mkononi, kawa kuwarubuni wananchi
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi Benjamin Kuzaga, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Agosti 18 mwaka huu kwenye maeneo ya Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi na jiji la Mbeya, ambapo katika upekuzi watu hao walikutwa na vitu mbalimbali ikiwemo simu, laptop, laini za simu 20 na vyeti vya watu
Aidha SACP Kuzaga Amesema watuhumiwa wawili kati yao wamekamatwa wakiwarubuni vijana kujiunga na kuwa wamiliki wenza wa kampuni ya Q NET yenye makao makuu nchini Malaysia, ambapo eneo la tukio walikutwa vijana 27, 8 kati yao ni wa kike na 19 ni wakiume wakichangishana fedha kwaajili ya kutuma kwenye kampuni ya Q NET ili waweze kupewa bidhaa zenye viini lishe na wao waweze kuuza kama watu wengine