Watu 80 wafariki katika shambulizi la Bomu lililowalenga washiha Iraq

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252


Vyombo vya usalama vya Iraq vimesema kwamba zaidi ya watu themanini wameuawa kwa shambulizi la bomu lililowalenga madhehebu ya kiislamu ya kishia kusini mwa mji wa Baghdad.

Gari lililokuwa limebeba vilipuzi hivyo lililipuka karibu na kituo cha mafuta ambapo watu wengi wa dhehebu hilo walikuwa wameegesha magari yao.

Wengi wa watu waliofariki ni wananchi wa Iran na Afghanistan.

Walikuwa wakitoka kwenye moja ya tukio muhimu la kidini kwenye mji mtakatifu wa Karbala



Askari wa kundi la kiislam wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.

kundi hilo la wapiganaji la kiislam mara kwa mara hulenga madhehebu ya kishia na kuwatuhumu kwamba ni waongo.

Chanzo:BBC Swahili
 
Wataisingizia Israel! Taarifa za awali ule moto uliowashwa na magaidi umezimwa na hakuna hata aliyejeruhiwa (MUNGU Mkubwa). Waarabu wamebaki kulipuana wao kwa wao tu.
 
Wataisingizia Israel! Taarifa za awali ule moto uliowashwa na magaidi umezimwa na hakuna hata aliyejeruhiwa (MUNGU Mkubwa). Waarabu wamebaki kulipuana wao kwa wao tu.
Roho mbaya haiwezi kukuacha salama kamwe itakuandama mpaka kaburini ndicho kinachowatafuna hawa Waarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…