Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Watu 7 familia moja wauawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana kuamkia leo Sima huko Sengerema, DC Terack athibitisha.
Uchunguzi waanza.
====================
Watu saba wa familia moja wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo (Jumatano) na chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.
Kufuatia mauaji hayo Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ametoa saa 48 kwa jeshi la polisi kuhakikisha linawakamata waliohusika na mauaji hayo na kuwafikisha katika vyombo vya sharia.
Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu ambaye jina lake limehifadhiwa wauaji hao walitekeleza mauaji hayo usiku wa manane wakiwa na mapanga na baada ya kufanya hivyo walitokomea kizani wakiwa wamevalia nguo nyeusi na kuficha nyuso zao.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limesema litahakikisha linawakamata wauaji hao na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Katika tukio hilo, watoto wawili wa familia hiyo walinusurika kuuawa baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
Chanzo: tbc