Watu 574 Wajitokeza Kuhakiki Silaha Dar es Salaam

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao.

Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa.

“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 90 zilizopangwa kumalizika” alisema.

Wakati huohuo, Siro alisema wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini.

“Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata na wale wanaojifanya madalali wao, wanashirikiana na majambazi hivyo nataka waache mara moja,” alisema.
 
Kwa taarifa hii naona kama wananchi wameanza kumuelewa mkuu wa mkoa.
GUN.png

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao.

Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa.

“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 90 zilizopangwa kumalizika” alisema.
Chanzo: Mwananchi

Wakati huohuo, Siro alisema wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini. “Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata na wale wanaojifanya madalali wap, wanashirikiana na majambazi hivyo nataka waache mara moja,” alisema.
 
kweli hakuna tena amani bongo watu wote hao wanamiliki silaha.

Swali: Je, wanafahamu kuzitumia hizo silaha?
 
Uhakiki wa hizi silaha muhimu. Ila zoezi hili lifanyike kwa umakini. Nadhani ni kipindi ambacho wamiliki halali wa silaha wasiotumia silaha zao katika matukio halali ukutana eneo moja na wanaomiliki silaha kihalali huku wakizitumia kwa matukio halali. Kwa hiyo ni rahisi kwa kundi la kwanza kujua aina ya silaha anayomiliki mtu ambaye pengine uwa ni mlengwa wao wa siku nyingi na hatimae kumfuatilia kuipora silaha hiyo (njiani wakati akitoka kwenye uhakiki au nyumbani kwake) au siku nyingine wakati wa kwenda kufanya tukio la uhalifu kwa huyo mtu wakajiandaa kutegemea na silaha waliyoiona kwa mlengwa wao wakati wa uhakiki.

Ikumbukwe kwamba umiliki wa silaha ni siri ya mtu lakini wakati wa usaili watu uanika silaha zao hadharani na hivyo kila mtu aliye pale kwenye uhakiki kwa muda huo kujua silaha ya mwenzake ikiwa ni pamoja na ya jirani, rafiki n.k.
 
Tupe na takwimu za wamiliki silaha Arusha tuwajue sbb nasikia uko ni kama mikanda ya kiunoni asiokuwa nao unamshangaa
 
Back
Top Bottom