Iran imewakamata watu 500 wanaotuhumiwa kushirikiana na maadui kwa kutoa taarifa nyeti, mkuu wa polisi wa nchi hiyo Ahmadreza Radan alisema Jumapili, wakati ndege za kivita za Israel na Marekani zikiendelea kushambulia malengo mapya ndani ya nchi hiyo.
Radan alisema takribani nusu ya kesi hizo zinahusisha matukio mazito, ikiwa ni pamoja na watu waliotoa taarifa zilizosaidia kulenga mashambulizi pamoja na wale waliorekodi picha au video za maeneo yaliyoshambuliwa na kuzituma kwa wengine. Hata hivyo hakutoa maelezo ya kina kuhusu muda halisi wa kukamatwa kwa watu hao.
Awali, vyombo vya habari vya Iran viliripoti kuwa watu kadhaa walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo siku ya Jumapili.
Kaskazini magharibi mwa Iran, shirika la habari la Tasnim News Agency liliripoti kuwa watu 20 walikamatwa kwa tuhuma za kutuma taarifa za maeneo ya vituo vya jeshi na usalama vya Iran kwa Israel, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa mkoa huo.
Katika eneo la kaskazini mashariki mwa Iran, ambalo halijaathiriwa sana na mashambulizi ya anga, Tasnim lilisema watu 10 pia walikamatwa, baadhi yao wakituhumiwa kukusanya taarifa kuhusu maeneo nyeti na miundombinu ya uchumi.
=============
Iran has arrested 500 people accused of sharing information with enemies, the Islamic Republic's police chief said on Sunday, as Israeli and U.S. fighter jets continue to strike new targets in the country.
Half of those cases had involved serious incidents "including people who provided information for hitting targets and individuals who took footage of strike locations and sent them," Ahmadreza Radan said, without going into detail on when the arrests took place. Earlier, Iranian media reported dozens of arrests in several regions on Sunday.
In northwestern Iran, the semi-official Tasnim news agency said 20 people were arrested on accusations by the provincial prosecutor's office of sending location details on Iran's military and security assets to Israel.
In northeastern Iran, which has remained relatively untouched by air strikes, Tasnim reported the arrest of 10 people, with some accused of collecting information on sensitive locations and economic infrastructure.
Source: Reuters